May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TanTrade yaendelea kupiga chapuo kwa wazalishaji wa Tanzania kuingia masoko ya kimataifa kupitia mikutano

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) imeendelea kupaisha makampuni ya Tanzania kupitia Maonesho yanayokwenda sambamba na program za Mikutano ya Mifumo ya usalama wa Chakula Afrika (AGRF2023) inayoendelea katika kituo cha JNICC Dar es salaam hadi tarehe 8 Septemba 2023.

Kampuni hizo zimepatiwa eneo maalum la Bazaar kupitia mwavuli wa TanTrade ambapo wanaonesha bidhaa za kimkakati zilizozalishwa na kufungashwa kukidhi viwango vya kimataifa ikiwemo Korosho, kahawa, chai, Nafaka na kokoa.Lengo Kuu ni kufungua masoko kwa kuhamasisha mauzo ya nje (exports), kusaidia kuongeza mapato ya fedha za kigeni, kuongeza ajira na ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.

Awali, miongoni mwa wadau muhimu na Viongozi mbalimbali waliotembelea ni pamoja na Mhe Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye alipongeza juhudi za kutangaza bidhaa za nchi na pia kutoa maoni kuwa Maonesho makubwa ya viwanda yanayotarajiwa Oktoba 2023 ya TIMEXPO yanayoandaliwa na TanTrade na CTI mialiko iwafikie wadau wa Njombe pia waweze kushiriki kikamilifu kwa kuwa ni fursa za kuonesha wanachozalisha, kuonana na wanunuzi watarajiwa na vile vile kuzitambulisha bidhaa mpya sokoni.