May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Vingunguti yabomoa safu ACT Wazalendo

Na Heri shaban, TimesMajira Online, Ilala

Chama cha Mapunduzi (CCM) kimeivunja safu ya chama cha upinzani cha ACT WAZALENDO kata ya vingunguti wilayani Ilala kwa kumchukua Meneja Kampeni wa ACT WAZALENDO Said Sultan Mazunga ,aliyetoka chama hicho na kujiunga ccm.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara vingunguti wilayani Ilala aliyekuwa meneja kampeni sultan Mazunga alisema amejiunga ccm kwa mapenzi yake mwenyewe kwenda kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara vingunguti wilayani Ilala uliokuwa unazungumzia maendeleo yaliofanywa na Serikali Diwani wa Kata ya Vingunguti ambaye ni meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, alisema nyumba 32 zinatarajia kubomolewa mtaa wa Majengo kwa ajili ya kujenga machinjio ndogo ya kuchoma nyama ya kisasa za biashara ya mbuzi .

“Mchakato tayari wa kuwalipa fidia nyumba hizo baada nyumba kubomolewa yatajengwa machinjio ndogo ya kuchoma nyama za kisasa nawaomba wananchi wa vingunguti wilayani Ilala muunge mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli”alisema Kumbilamoto

Akizungumzia maendeleo mengine yaliofanywa na Serikali ndani ya kata ya vingunguti alisema ujenzi wa Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ambayo imezinduliwa jana iliyogharimu shilingi million 128 na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pesa za sekta ya elimu kwa ajili ya madarasa wilayani Ilala ambapo kata ya vingunguti ametoa pesa za madarasa amewataka Ukanda wa gaza kuunga mkono maendeleo yanayofanywa na Serikali maendeleo hayana chama.

Katika hatua nyingine Meya Kumbilamoto alisema halmashauri ya jiji la Dar es Salaam inatarajia kujenga Ofisi ndogo ya Mapato ya Kanda namba tatu kata ya vingunguti kwa ajili ya ukusanyaji Mapato na kutoa huduma za Serikali kuwapunguzia wananchi mzigo wa kwenda halmashauri ambapo mchakato wa ujenzi huo umeanza.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Hashimu Jumbe, akitoa Salam za halmashauri ya jiji alisema halmashauri hiyo kwa sasa imegawanywa kanda saba amewataka wananchi wa Vingunguti kutoa ushirikiano huduma zote za Serikali zinafanyika vingunguti.

Hashimu Jumbe aliwataka wafanyabiashara wilayani Ilala wasifunge maduka yao waache maduka wazi halmashauri ya jiji kwa sasa inapita mtaani kuwa hakiki wafanyabiashara wote.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la segerea Lutha Lucharaba alisema maendeleo ya Vingunguti yanafanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Diwani wake Omary Kumbilamoto.

Lucharaba alisema Barabara za vingunguti zitajengwa za kisasa kwa kiwango cha lami na kuwekwa taa wana vingunguti waendelee kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali wakati wa uchaguzi ukifika wasifanye makosa wachague ccm kwa ajili ya maendeleo kura ya Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan ubunge Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na udiwani Omary Kumbilamoto.