April 23, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANROADS:Ushiriki wa wazawa kwenye miradi hauridhishi

Na Zena Mohamed,TimesmajiraOline,Dodoma

KAIMU Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS)Mhandisi Ephatar Mlavi ameeleza kuwa tathmini inaonesha kuwa ushiriki wa wazawa katika Miradi hauridhishi. Thamani ya miradi mikubwa inayotekelezwa na takribani ni takriban asilimia 10 tu.

Amesema kwa kutambua hilo serikali imeweka mkazo na kuchukua hatua mahususi kuongeza ushiriki wa wazawa katika utekelezaji wa miradi na matengenezo ya barabara na madaraja.

Mha.Mlavi ameeleza hayo jijini hapa leo Machi 30,2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari maendeleo ya utekelezaji wa majukumu  ya Wakala katika kuboresha miundombinu ya barabara ambapo ametaja mikakati hiyo ni kazi za matengenezo ya barabara na madaraja kwa asilimia 100 ziendelee kusimamiwa na Makandarasi Wazawa nakusimamiwa na Washauri Elekezi  kusimamiwa na Washauri Elekezi Wazawa tu. 

“Wastani  wa miradi 1,036 yenye thamani Zaidi ya Shilingi billioni 390 hutekelezwa na wazawa kila mwaka. Kuna mkakati wa Kutenga asilimia kumi (10%) ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa ajili ya Miradi ya mafunzo kwa vitendo. 

“Kuna miradi minne yenye thamani ya Shilingi bilioni 53.6 iliyotengwa mahususi na inatekelezwa nawakandarasi wanawake wazawa kama sehemu ya mafunzo,”amesema Mha.Mlavi

Mkakati mwingine amesema kutenga  angalau asilimia thelathini  ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa wazawa na makundi maalumu ya Vijana, Wazee, Wanawake na wenye mahitaji maalum.

Aidha amesema kuwa Serikali imeboresha sheria ya ununuzi wa umma kwa kuongeza wigo wa miradi iayotekelezwa kwa kutoa kipaumbele kwa wazawa toka bilioni 10 hadi bilioni 50.