April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya Hopepluss yatoa msaada muhimbili kwa watoto wenye usonji

Na Iddy Lugendo, TimesMajira Online

TAASISI ya Hopepluss imetoa msaada wa vitu kwaajili ya kusaidia baadhi watoto wenye usonji na ulemavu, vitu hivyo vyenye thamani ya jumla shilingi 956, 000/= katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili idara ya Utengamao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mei 27 jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Hopeplus Organization Abdallah Abdallah amesema lengo lao kuu nikuhakikisha watoa misaada kwa watu wenye ulemavu na wanapata mahitaji yao, fursa mbalimbali za kielimu, kijamii na kufikiwa na huduma zote ambazo zitasaidia kwa watu wenye ulemavu.

“lengo letu kuu nikuhakikisha tunatoa misaada kwa watu wenye ulemavu na wanapata mahitaji yao, fursa mbalimbali za kielimu, kijamii na kufikiwa na huduma zote ambazo zitasaidia katika ustawi wa watu wenye ulemavu katika kufika malengo hayo, tumefika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa misaada kwa watoto wenye Usonji (AUTISM) tumeleta Bima za Afya na Pampers”.alisema abdallah

“tumetoa msaada huu kwa namna moja ama nyingine kuweza kusaidia familia pamoja na watoto wenye ulemavu, sio huduma tu ya afya inayotolewa hapa katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili bali pia kusaidia familia hizi kupata mahitaji ya watoto hao na kujifunza kuhusu ugonjwa wa Usonji”. alisema abdallah

Aidha kaimu katibu Mkuu wa Hopeplus Organizantion Mickdad Uhuru amesema wamefanya tukio la hisani haswa lengo likiwa ni kuwasaidia watoto wenye usonji (AUTISM), pamoja na misaada hiyo ni Bima za Afya 15 kila bima moja yenye thamani ya 50,400 na Pampers zilizo katika ‘package’ 15.

“Msaada huu utakwenda kuwasaidia wakina mama na watoto, Tunaishukuru Hospitali ya taifa ya muhimbili kwa kutupa ushirikiano na vile tunaiomba jamii kushirikiana nasi kuhakikisha kwamba tunagusa makundi haya ya watoto ambayo kwa jamii yetu yamesahaulika”. alisema abdallah

Mmoja wa mwanachama Hopepluss Organization Happyness nadaki alisema tumejifunza mengi katika siku hii ya leo kupitia kutembelea hawa watoto wenye mahitaji maalumu, ugonjwa huu wa usonji unasumbua sana watoto, tunaishauri jamii waje kusaidia.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utengamao Muhimbili Abdallah Makala alisema mtu anaweza akawa mlemavu na bado akaweza kusoma na kufanya mambo mengine, waatalam wa afya tusiwanyanyapae walemavu wote tumetoka kwa mwenyezi mungu na tutarejea.

“Jumla ya shilingi 956,00 ikiwa ni pamoja na kadi za NHF 15 na Pampers, Tunaamini yakwamba msaada huu utawafikia walengwa na utakwenda kwa watoto na tutashirikiana kwa pamoja na tutajenga umoja”.alisema Makala

Mkuu wa Idara ya Utengamao Muhimbili Abdallah Makala akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada kutoka kwa Hopepluss Organization leo ijumaa mei 27, 2022.
Mwenyekiti wa Hopepluss organization Abdallah Abdallah akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada kwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili leo ijumaa mei 27, 2022.
Kaimu katibu Mkuu wa Hopepluss organization Mickdad Uhuru akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada kwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili leo ijumaa mei 27, 2022.
Mwanachama wa Hopepluss organization Happyness Ndaki akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada kwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili leo ijumaa mei 27, 2022.
Mwenyekiti wa Hopepluss Organization Abdallah Abdallah (kulia) akimkabidhi pampers mmoja wa wazazi (kushoto) leo ijumaa mei 27, 2022 Hospitali ya taifa ya muhimbili.
Baadhi ya wanachama wa Hopepluss organization baada ya kukabidhi msaada kwa watoto wenye usonji na ulemavu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili leo ijumaa mei 27, 2022.