December 7, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

St Anne Marie kumsomesha aliyeongoza kitaifa darssa la saba

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online,Dar

MWANAFUNZI aliyeongoza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba, Eluleki Haule, ameula baada ya shule aliyosoma ya St Anne Marie Academy kuahidi kumsomesha bure hadi kidato cha sita.

Ahadi hiyo ilitangazwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dkt. Jasson Rweikiza wakati wa hafla iliyoandaliwa na shule hiyo kumpongeza kutokana na ushindi wake.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Constansia Buhiya na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Kheri James.

Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akionyesha cheti alichokabidhiwa na shule yake ya St Anne Marie kumshukuru kwa kushika nafasi hiyo kwenye hafla ya kumpongeza iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mbezi Kimara kwa Msuguri Dar es Salaam

Dkt. Rweikiza alisema mbali na kumsomesha bure shule hiyo itampa sh. 3,000,000, kumpeleka kumtambulisha bungeni Dodoma yeye na wazazi wake na kubandika picha yake kwenye magari yote 51 ya shule hiyo.

Anewataka wanafunzi wahitimu kuacha kubweteka huku akiwasisitiza kusoma na kujituma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika kasomo yao na mitihani kwa ujumla.

“Niwashukuru walimu kwani walipambana sana hadi kufanikiwa kupata mafaninikio haya, pia nimshukuru Mkuu wa shule kwa uongozi boro pamoja na wanafunzi wote waliofanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yao na niwasisitize muendelee kusoma kwa bidii kwani taifa linawategemea,” alisema Rwaikize.

Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akimlisha keki Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Acdemy, Dk. Jasson Rweikiza wakati wa sherehe ya kumpongeza kwa kushika nafasi hiyo iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. Dkt. Rweikiza ameahidi kumsomesha hadi kidato cha sita.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James alimpongeza Eluleki Haule na kumtaka aendelee kufanya vizuri kwenye masomo yake ya sekondari.

Alisema kwa matokeo hayo ni ishara kwamba wazazi na walimu wanatimiza majukumu yao huku akitoa wito kwa wazazi walezi na jamii kuwalea watoto katika maadili mema na kutoa kipaumbele kwenye elimu ili badae wajisaidie na kulisaifia taifa kwa ujumla.

Mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, Eluleki Haule akikata keki katuka sherehe iliyoandaliwa na St Anne Marie kumpongeza kwa kufanikiwa kuwa wa kwamza kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu.

“Kwa niaba ya Serikali tunampongeza Kijana Haule kwa kuwa Tanzania one kwa mwaka huu. Leo Tanzania nzima wanaijadili St. Anne Marie kwasababu ya mtoto huyu, hii ni safari ya kwanza ambayo umeanza tunatarajia utafanya vizuri zaidi katika ngazi zinazoendelea,” alisema James.