Na Joyce Kasiki,Dodoma
SPIKA wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Bunge la Dunia (IPU) Dkt. Tulia Ackson (Mb) amezindua rasmi Bunge Marathon , litakalofanyika 13 April 2024 jijini Dodoma.
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Naibu Spika Mussa Zungu , Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Festo Sanga, Wabunge na Wadau mbali mbali wa michezo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dkt.Tulia amesema matukio yatakayofanyika katika Bunge Marathoni yatatoa fursa kwa wananchi kushiriki pamoja na wawakilishi wao bungeni na wadau mbalimbali katika mbio hizo.
Aidha amesema mbio hizo zitakuwa na malengo mahsusi ya kuchangisha rasilimali fedha na mali kwa lengo litakalokuwa limepangwa kila mwaka.
Kwa mujibu wa Dkt.Tulia ,lengo kuu la mabonza hayo ni kuhamasisha wabunge na watumishi wa ofisi ya Bunge klujenga tabia ya kufanya mazoezi kama wanafamilia wa taasisi ya Bunge.
Uzinduzi huo umefanyika 09 Novemba 2023, ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Bungeni Dodoma
More Stories
Kyobya: Watakaohusika kudhoofisha jitihada za Serikali,Pori la Akiba Kilombero kushughulikiwa
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu