May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyabiashara waaswa kutumia mifumo ya mauzo kuboresha biashara zao

Na Mwandishi wetu, timesmajira

WAFANYABIASHARA nchini wameaswa kutumia mifumo ya mauzo ya kidigitali(Smart Mauzo)ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa kumbukumbu ya taarifa za biashara na miradi mbalimbali wanayoiendesha na kuona faida na hasara zinazoweza kujitokeza kiuhalisia zaidi.

Ameyasema hayo Jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Teknolojia za kifedha kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere JNICC,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Oval Teknoloji inayojihusisha na utengenezaji wa mifumo mbalimbali ya kompyuta Ally Salum alisema mifumo hiyo imekuwa rahisi kwa jamii kutokana na maisha kwa sasa kubadilisha kuwa ya kidigitali.

Amesema mifumo hiyo ya kusimamia biashara na miradi imeenda kubadilisha maisha ya wafanyabiashara wengi kwa kuondokana na Analojia na kuingia kidigitali ambapo taarifa yoyote mtu anayoitaka kulipata kiharaka bila kupoteza kumbukumbu zozote.

“Mifumo hii inarahisisha mtu kupata taarifa za biashara kwa urahisi na kufanya maamuzi sahihi katika uagizaji wa mizigo au kujua mwenendo wa biashara,”amesema na kuongeza

“Kama nchi uwanda wa kidigitali kwa sasa umejua sana na sisi kama Kampuni tumeona kufikisha mifumo hii ili kuweza kurahisisha matumizi mazuri ya teknolojia ambayo itawasaidia kutumia teknolojia kwa wigo mpana na kufikia soko kubwa,”amesema.

Amesema licha ya nchi kupiga hatua kubwa katika ukuaji wa kidigitali hivyo kuna umuhimu wa kampuni za kiteknolojia kushirikiana ili kuhakikisha adhima ya serikali inatimia.

“Sisi ni mara yetu ya kwanza tangu kuanzishwa kwa kampuni yetu 2018 kushiriki maonesho haya lakini tumepata fursa ya kujifunza kwa wengine lakini pia fursa mbalimbali hivyo tutaendelea kushiriki maonesho haya kila mwaka,”amesema

Kwa Upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Oval Teknoloji,Latifa Guka amesema mifumo ya smart Mauzo kwa Wafanyabiashara ni msaada mkubwa kwa Wafanyabiashara katika kuhifadhi taarifa za biashara zao.

Amesema mfumo huo umekuwa na faida ya utunzaji taarifa na kutopotea kwa taarifa yoyote kupitia mifumo hiyo iliyosahihi kwaajili ya umuhimu wa biashara,ambapo kwa sasa Kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi nchi nzima wanafanya kazi Tanzania nzima.