May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Siku 365,Rais Samia ameendelea kuboresha afya Mwanza

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Katika kipindi cha mwaka mmoja (siku 365) za Rais Samia madarakani,amefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza ikiwemo afya.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya siku 365 za Rais Samia kwa Mkoa wa Mwanza katika hafla iliofanyika jijini Mwanza.

Mhandisi Robert,amebainisha kuwa ili kuhakikisha huduma za kibingwa zinaboreshwa katika kipindi hicho kumekuwa na uboreshaji wa huduma za kibingwa katika Mkoa wa Mwanza ambapo zaidi ya bilioni 4.9(4,962,082,500) zimetolekwa kwa ajili ya kuboresha huduma hizo katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Ambapo alielezea kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa ajili ya kuboresha miundombinu,kujenga majengo ya kutolea huduma za kibingwa,kuongeza vifaa vya uchunguzi na tiba kama x-ray,MRI,mammography kwa ajili ya uchunguzi sa saratani kwenye matiti,CT-scan na mashine za kutolea mionzi ya kutibu saratani katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando.

Zaidi ya bilioni 12.3(12,321,092,000) kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou-Toure,ili kutoa huduma za kibingwa kwa kujenga jengo la mama na mtoto, kumimika mashine ya X-ray,CT-scan na vifaa vya huduma za dharura.

Pia ameeleza kuwa katika kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za afya Mkoa wa Mwanza unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya afya,mbapo katika kipindi hicho Mkoa huo ulipokea kiasi cha bilioni 10.8 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya za Halmashauri ya Buchosa, Sengerema Misungwi,Kwimba na Ilemela.

Aidha amesema,Mkoa ulipokea kiasi cha bilioni 3.75 fedha za tozo ya miamala ya simu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 10,bilioni 1.35 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati 27 kwa Halmashauri zote zilizopo mkoani Mwanza.

Huku biilioni 2.7 kwa ajili ya upanuzi wa hospitali ya Nansio wilayani Ukerewe ili iweze kutoa huduma za kibingwa ambapo tayari Mkandarasi amekabidhiwa mradi.

“Hiyo ni baadhi ya miradi mikubwa inayotekelezwa kwa ujumla,miradi inayoendelea katika sekta ya afya Ina thamani ya zaidi ya bilioni 40,”amesema Mhandisi Gabriel.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya siku 365 za Rais Samia kwa Mkoa wa Mwanza katika hafla iliofanyika jijini Mwanza. (Picha na Judith Ferdinand)
Baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya kuwasilisha taarifa bya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya siku 365 za Rais Samia Mkoa wa Mwanza ilio wasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, hafla iliofanyika jijini Mwanza. (Picha na Judith Ferdinand)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,kulia akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla, akimkabidhi jarida maalumu la nchi yetu kuhusu mwaka mmoja wa Rais Samia na kitabu Cha taarifa ya miradi ya maendeleo Mkoa wa Mwanza kwa siku 365 za Rais madarakani,katika hafla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya siku 365 za Rais Samia kwa Mkoa wa Mwanza iliofanyika jijini Mwanza. (Picha na Judith Ferdinand)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel,kulia akimkabidhi Mwandishi wa Habari Benard James kwa niaba ya waandishi mkoanwa Mwanza, jarida maalumu la nchi yetu kuhusu mwaka mmoja wa Rais Samia na kitabu cha taarifa ya miradi ya maendeleo Mkoa wa Mwanza kwa siku 365 za Rais madarakani,katika hafla ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya siku 365 za Rais Samia kwa Mkoa wa Mwanza iliofanyika jijini Mwanza.(Picha na Judith Ferdinand)