Na Joyce Kasiki,Timesmajira online Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Utawala Bora Innocent Bashungwa amewataka wakuu wa mikoa nchini,kuwasilisha kwake taarifa ya ujenzi wa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 kabla ya Januari 22 mwaka huu.
Akifungua Barazala la wafanyakazi la Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).Bashungwa amesema kabla ya kuwasilisha taarifa hiyo lazima wajiridhishe kama fedha iliyotumika inalingana na kazi iliyofanyika.
Amesema ujenzi madarasa hayo unaenda kuongeza uandikishaji kuanzia darasa awali ,msingi na kidato cha kwanza huku akitoa pongezi kwa Rais Samia kufanikisha zoezi hilo la ujenzi wa madarasa 15,000.
“Rais wetu ameafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tunapambana na UVIKO 19 katika maeneno mbalimbali,katika eneo hili la ujenzi wa madarasa klkinaenda kuongeza uandikishaji wa wanafunzi na hivyo watoto wengi wameandikishwa mwaka huu,hivyo naomba wakuu wa mikoa waniletee taarifa ya ujenzi ambao unalingana na thamani ya fedha iliyotumika na siyo vinginevyo.”amesema Bashungwa na kuongheza kuwa
“Kutokana na ujenzi huu ,sasa watoto hawatembei umbali mrefu kufuata shule.”
Katika hatua nyingine amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuangalia namna ya kutatua kero za watumishi wake huku akitoa maelekezo kwa TSC kuanzisha dawati la wastaafu ambalo litakuwa na kazi ya kufuatilia mafao yao.
Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hili wafanye kazi weledi na bila kufumbia macho watumishi wanaokosa uadilifu katika utendaji wao wa kazi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato