May 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serengeti Lite, Uber watoa ofa watakaohudhuria Oktobafest

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Serengeti Breweries Limited imeungana na Uber kuwapatia ofa kabambe washiriki watakaosafiri kwenda kuhudhuria tamasha la Oktobafest.

Ushirikiano huo unalenga kuongeza chachu ya kusherehekea utamaduni wa Tanzania huku ukisaidia kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kuhakikisha usalama wa washiriki wote.

Tamasha la Oktobafest, ambalo limeandaliwa na Serengeti Breweries Limited, litafanyika kwenye viwanja vya Coco Beach leo. Tamasha hili la kipekee limejizatiti kutoa burudani ya kiutamaduni zaidi, kusherehekea utamaduni wa Tanzania kupitia bia, muziki, mitindo, na chakula.

Habari nzuri ya kuvutia zaidi katika Tamasha hilo ni punguzo maalum la 40% kwa safari zote za Uber kwenda na kutoka Oktobafest.

Kupitia Kampeni ya Inawezekana, Kampuni ya Serengeti Breweries Limited imejitolea kuhamasisha unywaji wa kistaarabu, kuhakikisha kwamba washiriki wanafurahia tamasha kwa kistaarabu na hawaweki hatarini usalama wao.

Akizungumzia Tamasha hilo, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited, Rispa Hatibu amesema lengo la kuandaa Oktobafest ni kuonesha Tamaduni mbalimbali Tanzania.

“Serengeti Lite kuandaa Oktobafest, tukio linalosherehekea tamaduni mbalimbali za Tanzania, na tunafurahi kushirikiana na Uber katika jitihada hii. Tunataka washiriki wetu kufurahia tamasha kwa kistaarabu na kwa usalama, na ushirikiano huu unatusaidia kufikia lengo hilo,” amesema Hatibu.

Naye Meneja wa Uendeshaji wa Uber nchini Tanzania, Monica Mziray amesema, “Kwetu Uber, tunajitahidi kutoa njia za usafiri zilizo rahisi na salama.

“Ushirikiano wetu na Serengeti Lite kwenye Oktobafest unakwenda sambamba na dhamira yetu. Tunataka wapenzi wa tamasha hili wafurahie wakiwa kwenye tamasha hili huku wakifanya maamuzi ya kistaarabu na kuhakikisha usalama wao kipindi chote cha tamasha,” amesema.

Ushirikiano huo wa kimkakati kati ya Uber na Serengeti Lite si tu ni uthibitisho wa dhamira yao kwa jamii, bali pia ni njia ya kuwapatia wasaa wa kipekee wa washiriki wa tamasha hili.

Kwa punguzo la kipekee la Uber, washiriki wataweza kusafiri kwenda na kurudi kutoka Coco Beach kwa urahisi, kuepuka hatari za kuendesha wakiwa wamekunywa pombe na kwa usalama wao.

Oktobafest, kama tamasha, linalenga kuunganisha mambo mbalimbali yaliyomo kwenye utamaduni wa Tanzania. Kupitia Kampeni ya Inawezekana ya Serengeti Breweries Limited inahamasisha kutoendesha chombo cha moto ukiwa umekunywa pombe na kutumia safari salama zinazopatikana kupitia Uber, washiriki wanaweza kufurahia tamasha hili la kitamaduni bila wasiwasi wowote.