May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rutenge Mkurugenzi mpya FCS

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Shirika la The Foundation For Civil Society (FCS), limemchagua Justice Rutenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji katika shirika hilo ambaye anatarajiwa kuanza kazi rasmi Mei mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS aliyemaliza muda wake wa uongozi, Francis Kiwanga wakati akimkabidhi ofisini Mkurugenzi Mtendaji huyo mpya Machi 5,mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi nyaraka za Ofisi na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo Justice Rutenge,hafla hiyo imefanyika Machi 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

Kiwaga amesema licha ya kuwa anamaliza muda wake amehahidi kuendeleza ushiriano na Shirika hilo na atakuwa balozi kwa kutoa mchango wake pindi atakapohitajika.

Aidha Kiwanga amesema shirika hilo linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya demokrasia na uhuru wa watu.

Ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

“Kwetu sisi tunaona ni taasisi inayopigania misingi ya utawala bora, tunahitaji kuendeleza juhudi za kupambania maendeleo ya watu, na hili ni suala la kujikumbusha kila siku,” amesema Kiwanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS, anayemaliza muda wake wa uongozi Bw. Francis Kiwanga (kulia), akimkabidhi nyaraka za Ofisi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo, Justice Rutenge (kushoto), katika hafla fupi ya makabidhiano ya uongozi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika Machi 5, 2024 Jijini Dar es Salaam. (Katikati), ni Mwenyekiti wa Bodi ya FCS Bw. Ali Laai

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya FCS, DKt. Ally Laay, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake kwa kuwa mchapakazi, mwadilifu na kusimamia majukumu yake kwa weledi na kuiheshimisha FCS.

Pia, amesema kuwa ana imani kubwa na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake mei mosi, 2024.

“Bwana Rutenge ameshinda kwa kishido kikubwa licha ya kuwepo ushindani mkubwa katika mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya, bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea aliposhia kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana” amesema Laay.

Naye Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge, ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na Watumishi wa FCS wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Ally Laay muda mfupi kabla ya kufanyika makabidhiano ya nyaraka za ofisi kati ya Francis Kiwanga, Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa taasisi hiyo, Justice Rutenge.
Mwenyekiti wa Bodi ya FCS, DKt. Ally Laay, (kulia), akielezea mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo (Kushoto), ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge.