April 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RPC Ilala awatetea wanaume wanaonyimwa unyumba

Na Heri Shaaban

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Magiligimba, amesema wanaume wote waliopo Wilaya ya Ilala wakinyimwa tendo la ndoa na wake zao watoe taarifa Polisi katika madawati ya Jinsia kwa ajili ya kuwachukulia hatua wanawake .

Kamanda Debora aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Tabata

“Nina omba wanaume wanaonyimwa unyumba kuripoti katika madawati ya jinsia yaliyopo katika vituo vya polisi kwani huo ni ukatili uwezi kumfanyia hivyo mweza wakati mkiwa ndani mke na mume”alisema Debora

Alisema katika maadhimisho haya ya siku 16 za Kupinga Ukatili yaliyofanyika katika viwanja vya Tabata shule ambapo pia alikabidhi vitambulisho maalumu kwa madereva bodaboda na bajaji ili iwe rahisi kutambulika.

Alisema kunyimwa unyumba husababisha kupata ukatili wa kisaikolojia yanapotokea hayo nendeni dawati la jinsia mripoti nasikia mnauliza mnaanzaje aliwataka wafike katiks madawati hayo watasikilizwa

Aidha amewataka bodaboda wa Ukanda wa Tabata ,Kimanga na Liwiti kujichunguza wao kwa wao ili kuwabaini wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema madereva bodaboda na bajaji kutoka maeneo ya Tabata, Kimanga na Liwiti wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kutokomeza vitendo vya ukatili wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Tabata.

Wakati huo huo Kamanda Debora alimpongeza mkuu wa kituo cha Polisi Tabata Mrakibu wa Polisi Cole Senkondo kwa ubunifu wake na kuweka mikakati ya Ulinzi na Usalama vizuri kwa kuwashirikisha jamii na madereva wa bodaboda .

Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Mrakibu wa Polisi Mosi Ndozero, alisema kuna ukatili katika vyombo vya usafiri ndiyo maana walilenga kutoa elimu kwa bodaboda.

“Unamvizia mtoto wa shule kisha unampa lifti au kinamama wa watu mnawapeleka sokoni siku ya pili unamrubuni huo ni ukatili tuache,”alisema Mosi.

Awali Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata Mrakibu wa Polisi, Colle Senkondo, alisema waliamua kuandaa vitambulisho maalumu vya madereva bodaboda na bajaji wa Kata za Tabata, Kimanga na Liwiti ili kudhibiti vitendo vya uhalifu.

“Kulikuwa na matukio mengi yaliyosababisha bodaboda kuchomwa moto na baada ya kufanya uchunguzi tulibaini si wakazi wa Tabata, ndiyo maana tuliamua tuwe na vitambulisho maalumu,” alisema Colle.