May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Kafulila Kurithi wajane, ngono zembe vichocheo vya UKIMWI

Na Heri Shaaban

MKUU wa Mkoa Simiyu David Kafulila, amesema vichocheo vya UKIMWI mkoani Simiyu ni wenza wengi, Kurithi wajane,kuanza ngono katika umri mdogo, kujihusisha na makundi hatarishi,kulewa kupindukia,kutumia Dawa za kulevya, idadi ndogo ya wanaume wenye tohara na biashara ya ngono.

Mkuu wa Mkoa Kafulila alisema amepata taarifa baadhi ya wadada wanadaiwa wanajiuza maeneo mbalimbali na hivyo akatoa maelekezo kwa wakuu wote wa Wilaya kuhakikisha maeneo yote yanayotumika kwa biashara ya ngono yanadhibitiwa, kwani hiyo sio biashara halali, na sio utamaduni wa nchi yetu..

Amewataka vijana wa mkoa huo na wadada wasijiushishe na ngono zembe ,ngono katika umri mdogo na makundi ya madawa ya kulevya kwani yanachangia vichocheo vya maambukizi ya UKIMWI.
.
Akizungumza katila madhimisho ya kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja Vya Halmashauri Bariadi, Mkoani Simiyu David Kafulila alisema toka miaka ya 1980 wakati janga la UKIMWI lilipoikumba Dunia, Dunia imefanikisha kwa kiasi kikubwa kupambana na janga hili,ili hali Changamoto kubwa ikiwa imebakia katika nchi zilizopo kusini mwa Jangwani la Sahara .

Kafulila alisema Dunia Inaendelea kupambana na jangwa la ukimwi kwa Sababu athari zake ni kubwa,nazo huathiiri mtu mmoja mmoja, familia na hadi Taifa.

” Mkoani Simiyu idadi ya maambukizi ya UKIMWI ni asilimia 3.9% ambayo ni chini ya kiwango cha Kimataifa ambacho ni asilimia 5.1%,hii inaonyesha kwamba kazi imefanyika.Lakini hii haimaniishi kwamba tulane badala yake tuzidishe mapambano, na iwe agenda kwenye vikao vyetu kuanzia ngazi ya kata “alisema Kafulila

Alisema vikao vya kamati ya maendeleo ni vyema vikajadili suala hili Mabaraza ya Madiwani RMO,kwenye vikao vyote vya RCC,DCC na vikao vya Madiwani mada kuhusu magonjwa ya UKIMWI na UVIKO namna na jinsi ya kujikinga ni lazima ziwe agenda za mawasiliano.

Alieleza kuwa tukijenga uelewa mzuri kuhusu magonjwa haya tuna uwezo mkubwa wa kujikinga na hatimaye kuepukana magonjwa yote hayo ujumbe wa Mwaka huu wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani unasema “ZINGATIA USAWA, TOKOMEZA UKIMWI, TOKOMEZA MAGONJWA YA MLIPUKO”. Kauli mbiu hii ni pana na inabeba mambo mengi.Kama viongozi tunapaswa kuzungumzia magonjwa haya ya mlipuko.

Asilimia 43% ya maambukizi mapya Tanzania, yanatokea kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-24, hii ndio nguvu kazi ya nchi ,hali hii inaonyesha kuwa tusipochukua hatua, tutabaki na Taifa dhaifu sana, kwani huwezi kujenga Taifa lenye nguvu kama lina vijana wenye afya dhaifu.

Alitoa wito pale ambapo itakuwa umeathirika huo sio mwisho wa maisha yako kupata ukimwi haimaanishi ni mwisho wa maisha yako na mwisho wa kufanya kazi hivyo aliwataka wajitahidi kukabiliana na janga hilo.

Pia aliwataka wawahi kupima ili tujue afya zao mapema kwani kwa kuwahi kutumia dawa sahihi na kwa usahihi kutafubaza kiwahi wadudu wa UKIMWI.

Kafulika alionya tabia ya wanaume kutegemea wake zao kupima VVU na kuamini kwamba majibu ya mke wake ni majibu ya wote kwani kufanya hivyo sawa na dhana potofu na wanaume tunatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kujua afya zao.

Mkuu wa Mkoa alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutilia mkazo agenda ya afya kwani imekuwa kipaumbele kikubwa sana katika serikali ya awamu ya sita.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akiwa katika viwanja vya Bariadi jana kwenye madhimisho ya Kilele cha siku ya UKIMWI Duniani (kulia)Katibu Tawala Prisca Kayombo
Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akizungumza na wananchi wa mkoa Simiyu viwanja vya Bariadi jana