November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia kuzindua matokeo sita ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka ya 2022, Oktoba mwishoni

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Dar es Salaam 

SERIKALI  imesema kuwa matokeo sita ya Sensa  ya Watu na Makazi ya Mwaka ya  2022  yamekamilika na yanatarajia kuzindua rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia imesema hadi sasa maandalizi ya zoezi hilo la Utangazaji wa matokeo yanaendelea vizuri na yatakapotangazwa yatabandikwa katika mbao za matangazo katika maeneo ya vijijini  ambayo ni pamoja na Kata/Shehia,Kijiji/Mtaa na Vitongoji. 

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam,Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022,Kamisaa wa sensa ya watu na makazi 2022, Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda alisema tangu kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu,wataalamu wao wamekuwa wakiendelea na kazi ya uchakataji wa taarifa zilizokusanywa ili kupata matokeo mbalimbali ya sensa hiyo.

Amesema kwa Sensa ya mwaka 2022  ambayo imetumia teknolojia ya hali ya juu iliyohusishs matumizi ya vishikwambi katika awamu zote z utekelezaji, imeweza kusaidia kukamilisha zoezi la kuhesabu watu,uchakataji na kuongeza ubora wa takwimu zilizokusanywa.

“Kutokana na mabadiliko ya teknolojia Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2002 na ile ya mwaka 2012 ambazo zilitumia teknolojia ya usomaji wa vivuli (scanning Technology )matokeo ya Sensa hizi yalikuwa tayari na  yalizinduliwa rasmi miezi mitatu  baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu,”amesema na kuongeza

“Kwa wakati huo nchi ilikuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zilifanikiwa kutoa matokeo ya mwanzo muda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu,”amesema.

Amesema ni utaratibu wa kimataifa kwamba baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu kazi zinazotakiwa kufanyika ni kuchakata matokeo ya Sensa na hatimaye kutoa matokeo ya mwanzo  muda mfupi baada  ya kukamilika kwa  zoezi kuhesabu watu.”Kwa wakati huo nchi yetu ilikuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zilifanikiwa kutoa matokeo ya mwanzo mkwuda mfupi baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu,”amesisitiza. 

Kwa Upande wake Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Mohamed Haji Hamza  ,amewashukuru Wananchi kwa namna walivyojitoa kuhakikisha Sensa ya watu na makazi ,Sensa ya majengo na Sensa ya Anwani za Makazi ya mwaka 2022 kufanikiwa. 

“Serikali inavishukuru vyombo vyote vya habari kwa kazi nzuri mlioifanya katika kipindi chote cha utekelezaji wa zoezi la Sensa na kufanikisha kuhesabu watu kwa asilimia 99.99 hivyo serikali itaendelea kuwahusisha katika kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu matumizi ya matokeo ya Sensa katika mipango jumuishi kwa maendeleo endelevu ya taifa,”amesema