May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia amlilia Anna Mghwira

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kilichotokea jana katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, leo jijini Dar es Salaam imesema; “

Rais Samia amepokea taarifa za kifo cha Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa taifa.”

Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina.