May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Samia Mgeni rasmi katika ufungaji wa lango la handaki mchepuko

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika tukio la kushuhudia ufungaji wa lango la handaki mchepuko (vaani diversion tunnel) ili kuruhusu maji yaanze kujaa katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Tukio hilo litafanyika siku ya Alhamisi, tarehe 22 Disemba 2022, Akizungumza na Waandishi wa habari leo Disemba 18 2022 Waziri wa Nishati January Makamba amesema kuwa Mpaka mwezi Novemba 2022 mradi umefikia asilimia 78.68.

Waziri Makamba ameeleza pia mradi huu una hatua kubwa mbili ambazo zina hadhi ya kushuhudiwa na kusherehekewa. Moja ni kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji na ya pili ni kuwasha mitambo ya kufua umeme.

Waziri Makamba amesema “Tunategemea itachukua misimu miwili ya mvua kulijaza bwawa na kuanza kujaribu mitambo”- Makamba.

Bwawa la Mwalimu Nyerere linahifadhi lita 33.2 bilioni za maji na kama zikitumika na mitambo yote, itaweza kuendesha mitambo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Faida ya mradi huu ni kilimo chini ya mto Rufiji, kuondoa mafuriko na kupata umeme wa uhakika.

Wananchi wanakaribishwa tukio hili litaonyeshwa mubashara kupiti vyombo mbalimbali vya habari.