May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti Mtemvu: Pesa za Tozo zimeleta maendeleo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu, amesema pesa za makato ya tozo zimeiletea Maendeleo makubwa ya nchi kwa kuibua miradi mbalimbali ya Maendeleo Mwenyekiti Abas Mtemvu, aliyasema hayo Jimbo la Ilala wakati wa kuzindua Barabara ya Kasongo iliyojengwa kwa fedha za tozo shilingi milioni 500 ambazo zilitolewa Kila Jimbo.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa toka apokee kijiti katika kuongoza nchini nchi yetu imepata miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo miradi ya sekta ya Afya Barabara ,miradi ya Elimu kwa kutumia pesa za tozo “alisema Mtemvu .

Amewataka Wana CCM Mkoa Dar ea Salaam kuunga mkono Juhudi za Maendeleo ambazo zinafanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kujenga nchi na kukuza sekta ya uchumi .

Aliwataka Wana CCM wenye kero ambazo zimeshindikana wawasilishe ofisini kwake CCM Mkoa kwa ajili ya Utatuzi wake .

Wakati huo huo alisema Januari Mwaka 2023 anatarajia kufanya mkutano mkubwa na Watendaji wa Serikali ,Wakuu wa Wilaya ,Mkuu wa Mkoa ,Meya wote ,Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu alimpongeza, Diwani wa Ilala Saady Khimji na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Ally Mshauri kwa kuandaa mkutano huo wa Maendeleo Mbunge Zungu aliwataka Madiwani na Wenyeviti wa jimbo la Ilala kila wanapofanya Shughuli za chama zikiwemo za Uwasilishaji Ilani wawashrikishe viongozi wa chama waweze kujionea matunda ya Serikali yao .

Mbunge Zungu alisema katika Jimbo hilo la Ilala pesa za Tozo zimeweza kuleta maendeleo makubwa kwa kufanya kazi mbalimbali Miundombinu ya Barabara ,kituo cha Afya cha kisasa Mchikichini ,madarasa Ilala .

“Katika Jimbo langu la Ilala Barabara ndio kero kubwa zikiwemo Barabara za Tukuyu,Tabora ,Utete katika uongozi wa Rais Samia zote zitatekelezwa katika utekelezaji wa Ilani na Rais wetu Samia Suluhu Hassan.”alisema Zungu .

Diwani wa Kata ya Ilala Saady Khimji alisema Mtaa wa Mafuruko ni mmoja ya Mitaa Mitano iliyopo Kata ya Ilala ambayo Ina wakazi 5117 Mtaa huo umepakana na wilaya ya Temeke kwa upande wa Kusini Kaskazini Diwani Kimji alisema Wananchi wa Mtaa wa Mafuriko Kata ya Ilala wana furaha kubwa kujengewa Barabara hiyo ambayo ilikuwa kero na kuanza Ujenzi wa Barabara za Boom na Gereji ambazo zitajengwa kwa kiwango cha Lami .

“Jimbo la Ilala Maendeleo yote yanaletwa na Mbunge wetu Mussa Zungu kiasi kikubwa Cha Barabara za Mitaa Mafuriko ndani ya Miaka miwili zitakuwa na Lami na zingine zitajengwa na mradi wa kuboresha miundombinu ya Jiji DMDP “alisema Khimji .

Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Ilala Said Sidde alisema Kata ya Ilala imepiga hatua kubwa Sana ya Maendeleo ambayo yanafanywa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na Diwani wake Saady Kimji Amewataka Wananchi viongozi wa chama kushirikiana na Serikali yao kwa ajili ya kujenga nchi .

Diwani wa Ilala SAADY KIMJI akikabidhi hotuba Kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam Abas Mtemvu Wakati wa kufungua barabara ya Kasongo Iliyopo Bungoni (Picha na Heri Shaaban )
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza na Wakazi wa Jimbo la Ilala Eneo la Bungoni wakati wa kuzindua Barabara ya Kasongo (Picha na Heri Shaaban )
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu ,Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,Diwani wa Ilala SAADY KIMJI na viongozi wa Chama wakifungua Barabara ya Kasongo Ilala (Picha na Heri Shaaban )
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu akikabidhi cheti Cha Shukrani Mdau wa Maendeleo Ilala Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi Halmashauri ya Jiji Sauda Rajabu Urasa (Kulia )Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (Picha na Heri Shaaban )
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu akizungumza na Wakazi wa Ilala Jana wakati wa kufungua barabara ya Kasongo (Picha na Heri Shaaban)