May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Chissano apongeza Tuzo ya Taifa ya Mwl. Nyerere

Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Msumbiji Joaquim Chissano akizungumza katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa nguli wa vitabu vya Riwaya nchini Richard Mabala akiwa katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Wahamasishaji wa Uandishi bunifu wakiongoza hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

RAIS mstaafu wa awamu ya pili wa msumbiji Joaquim Chissano ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuanzisha tuzo ya taifa ya mwalimu nyerere ya uandishi bunifu ambapo amesema itasaidi kuuza na kuenzi lugha adhimu ya kiswahili kwa nchi za Afrika ili kuendeleza matumizi kwenye maeneo muhimu ya kiutawala na kijamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Aprili 13, 2023 jijini Dar es Salaam Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano amesema kiswahili ni tunu na utambulisho wa afrika na mwafrika

“Juhudi za kutambua mchango wa wadau wa maandiko bunifu kwa lugha ya kiswahili ni muhimu na kwamba juhudi hizi ziendelezwe kwani uhai wa lugha yoyote duniani ni kuwapo na machapisho yaliyoandikwa kwa lugha hiyo” amesema Rais Mstaafu Chissano

“Ni wazi Mwl. Nyerere kwa dhati kabisa aliikuza lugha ya kiswahili kwa kuandika maandiko bunifu kama riwaya, mashairi na kutafsiri kazi mbalimbali za fasihi ya kingereza katika kiswahili hivyo ni heshima kubwa tuzo hii kupewa jina lake,” amesema Rais Mstaafu Chissano

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wizara imejipanga kuhakikisha utoaji tuzo za uandishi bunifu unakuwa endelevu na kwamba itahusisha nyanja mbalimbali ikiwemo uandishi wa vitabu vya watoto ili kujenga tabia ya watoto kujisomea wakiwa wadogo na zitakuwa zikitolewa kila mwaka Aprili 13.

Amesema lengo la tuzo hizo ni kuwatambua na kuwazawadia waandishi bunifu mahiri katika nyanja mbalimbali, kukuza lugha ya taifa ya Kiswahili, vipaji vya uandishi bunifu kwa Watanzania, kuongeza hamasa ya Watanzania kujisomea, kuhifadhi historia, amali na kukuza sekta ya uchapishaji na hifadhi za vitabu kwa shule, vyuo na maktaba zetu.