Na Mwandishi Wetu, Arusha
Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amezipongeza baadhi ya taasisi za umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuweza kuwafikia wananchi kiurahisi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA.
Ndejembi aliyasema hayo jijini hapa katika hotuba yake ya ufunguzi sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini
“Leo nimejionea kwenye mabanda pale PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda Hivyo nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji kulipeleka mbele taifa letu kimaendeleo. Na katika hili nitoe pongezi pia kwa taasisi ambazo tayari zimeweza kuwafikia wananchi kiurahisi Zaidi na kuondoa urasimu wa makaratasi…” alisema Mhe. Ndejembi
Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka. PSSSF ina huduma za PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi ni suluhisho kwa wanachama, wastaafu na waajiri kuweza kupata huduma popote walipo na muda wowote kwa kutumia simu janja au kompyuta bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za PSSSF.
More Stories
Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu latakiwa kutoa huduma bora za kisheria
Korea yaonesha utayari kuwekeza nchini katika uendelezaji wa madini mkakati
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500