December 7, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Phil Foden kuikosa fainali ya Euro 2020 leo dhidi ya Italia

LONDON, England

KIUNGO wa timu ya Taifa ya England, Phil Foden huwenda

akaukosa mchezo wa fainali ya Kombe la Mataifa Ulaya

(Euro 2020)

dhidi ya Italia utakaochezwa leo jioni

kwenye Dimba la Wembley nchini Uingereza,baada ya

kupata jeraha la mguu.

Foden, mwenye umri wa miaka 21 alikuja kama mbadala wa

wachezaji watatu katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya

Denmark Jumatano jioni hatua ya nusu fainali,

lakini

mchezaji huyo alimumia mguu.

Kwa mujibu wa BBC Sport, inaripoti kwamba Foden

alionekana kutofanya

Mazoezi ya mwisho kabla ya Fainali

ya Mashindano ya Uropa, na sasa inaonekana kuwa

mashakani kucheza fainali hiyo leo.

Kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate

amekiri kwamba

wataalamu wa matibabu watalazimika

‘kutathmini’kuona ikiwa anaweza kucheza au hatashindwa.
Ana jeraha la mguu,Lakini italazimika kutathmini hilo

baadaye.