May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yashiriki uwekaji wa jiwe la msingi SGR

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kama ilivyokuwa katika miradi mbalimbali ya kimkakati, Benki ya NMB imeendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa ushirikiano kwa Serikali na Wakandarasi ili kuhakikisha miradi inayojengwa kwa manufaa ya Watanzania inakamilika kwa wakati.

Katika mradi wa reli ya kisasa ya SGR, Benki ya NMB imeshiriki katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika awamu ya tatu ya ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 368 kutoka Makutupora mpaka Tabora. Mbali na kuwa wabia katika mradi huu mkubwa, benki hiyo imedhamini shughuli hii ya uwekaji wa jiwe la msingi iliofanyika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora.

Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB – Emmanuel Akonaay akimuelezea Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, jinsi benki ya NMB ilivyoshiriki katika mradi wa SGR kupitia wakandarasi wa mradi huo kwanzia Dar- Morogoro, Morogora- Dodoma mpaka sasa, Makutupora- Tabora. Pia, namna benki ilivyowawezesha wazabuni wa mradi huo kwa kuwapa mitaji na kuhakikisha watumishi wanalipwa kupitia Benki ya NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse(kulia), akizungumza na wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB waliofika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora kwa ajili ya kuuza na kuonesha bidhaa zao ambao pia wengi ni wazabuni katika mradi wa SGR
Wateja wa NMB wakipata huduma mbalimbali katika banda la benki hiyo katika viwanja vya Cheyo B.
Â