Na.Mwandishi wetu,Timesmajira
Benki ya NMB imetoa zaidi ya Sh180 bilioni kufadhili wafugaji na biashara katika mnyororo wa thamani wa mifugo, ikiwemo unenepeshaji, uzalishaji wa malisho, ununuzi wa mbegu bora na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, amesema hayo katika ufunguzi wa Tri-Nations Livestock Expo 2026 uliofanywa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, katika viwanja vya Mbogo Ranches, Ubena Zomozi, Chalinze. NMB ni mdhamini mkuu kwa mwaka wa nne mfululizo.
Mponzi amesema mikopo hiyo inatolewa kwa riba nafuu ya asilimia tisa, huku mkakati wa NMB wa agribusiness na agri-wholesale ukilenga kufadhili wafugaji, wazalishaji wa malisho, wanunuzi, wasindikaji na biashara kubwa katika sekta hiyo.

Dk. Nchemba amewataka wafugaji kutumia elimu na teknolojia inayopatikana katika maonesho hayo kukabiliana na uhaba wa malisho na kuongeza tija.
NMB imesema itaendelea kutoa elimu ya fedha, ushauri wa biashara, mikopo na bima kupitia matawi 248, mawakala zaidi ya 75,000 na huduma za kidijitali ili kusogeza huduma karibu zaidi na wafugaji nchini.



More Stories
Wananchi watakiwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi
Ujuzi wa vitendo nguzo ya kujitegemea
Mahundi ahimiza ushiriki kujenga,kulinda miradi