Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
AFRIKA inashuhudia visa pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19 vikiongezeka, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti juzi.
BBC imepitia hali ilivyo barani Afrika kutokana na ugonjwa huo unaosababishwa na Virusi vya Corona, na imechunguza nchi ambazo ziko katika hofu zaidi dhidi ya janga hilo:
VIRUSI VYA CORONA VINAENEA KWA KIASI GANI
Kwa kuwianisha na idadi za viashiria vyote, Afrika kwa sasa inahusishwa na kiasi kidogo tu ya visa vyote duniani, lakini viwango vya maambukizi kwenye baadhi ya nchi viko katika viashiria vya hofu ya kuongezeka kwa mamlaka za afya barani.
Wakati ilichukua karibu siku 100 kwa Afrika kufikisha idadi ya visa 100,000 vya Covid-19, ilitumia siku 18 tu matukio ya ugonjwa huo kutimia 200,000. Bado idadi iliongezeka tena mara mbili zaidi kufikia 400,000 katika muda wa siku 20 zilizofuata.
Muelekeo wa kuongezeka visa vya Covid-19 Afrika unaanza kufanana na maeneo mengine duniani ambako kumeathiriwa vibaya na Virusi vya Corona.
Nchi nyingi barani hivi sasa kunakabiliwa na maambukizi ya ugonjwa huo kwenye jamii, kulingana na WHO.
Hatua hiyo ni wakati mtu huambukizwa Covid-19 bila ya kuwa amekutana na mtu aliyethibitishwa alikuja na maambukizi kutoka nje ya nchi ama kwenye jamii anakoishi, mazingira ambayo husababisha ugumu kwa mamlaka husika kufuatilia ambako umeanzia eneo husika.
WAPI KULIKO SHAMBULIWA ZAIDI AFRIKA
Nchi mbili ambako kuna visa vingi zaidi vya covid-19 barani Afrika ni Afrika Kusini na Misri. Kunahusishwa na matukio mapya asilimia 60 yaliyoripotiwa Juni,mwaka huu.
Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya visa vya Covid-19 kwenye jumla matukio yaliyosajiliwa barani humo, wakati Misri ina idadi kubwa ya waliofariki kwa ugonjwa huo.
Nchini Afrika Kusini ambako Machi, mwaka huu, walipitisha moja ya hatua kali zaidi kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo ‘lockdowns’ kumeshuhudiwa visa vya covid-19 vikiongezeka kwa kasi baada ya kupunguza makali ya lockdowns hizo mwanzoni mwa Mei.
Jimbo la Western Cape (ambamo Jiji la Cape Town limo) kunahusishwa na karibu nusu ya visa vyote pamoja na zaidi ya nusu ya matukio yote ya vifo nchini humo.
Misri pia kumeshuhudiwa idadi ya visa vya ugonjwa huo ikiongezeka tangu katikati ya Mei, mwaka huu, lakini kuna viashiria ambavyo sasa inawezekana covid-19 imefikia kilele kutokana na taarifa za maambukizi mapya yanayotafsirisha kuwa yanapungua kidogo, ambayo yalisajiliwa mwanzoni mwa mwezi huu ‘Julai’.
Vilevile, kuna hofu kuhusu hali inavyoendelea nchini Nigeria, ambako wanashika nafasi ya pili kwa kusajili visa vingi zaidi vya vifo vya covid-19 Afrika baada ya Afrika Kusini,kulingana na ripoti ya WHO ya Julai Mosi, mwaka huu.
Mauritani pia kumeshuhudiwa ongezeko la kasi la visa vya ugonjwa huo wiki za karibuni.Inamaanisha kusisitizwa kuwa baadhi ya maeneo ya Afrika kumeshuhudiwa uwiano wa visa vichahe, kama vile sehemu za Afrika Mashariki.
Ripoti ya WHO Afrika iliyotolewa mara ya mwisho imeonesha kuwa nchi 10 tu barani kunahusishwa na zaidi ya asilimia 80 ya matukio yote yaliyoripotiwa eneo lake.
IDADI YA WANAOPOTEZA MAISHA AFRIKA
Idadi ya wastani wa vifo barani kwa ujumla imekuwa kidogo ikilinganishwa na maeneo mengine duniani, ingawa kuna miundombinu hafifu na isiyorasimishwa mingi kwenye nchi za Afrika.
WHO wanasema kuwa hali hiyo inawezekana kiasi fulani ni kutokana na idadi ya vijana barani, ambamo zaidi ya asilimia 60 ni wenye umri chini ya miaka 25.
Covid-19 inaamanika kusababisha vifo vingi zaidi kwa watu wenye umri mkubwa.
Upande mwingine wa kumulika wastani wa vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni kuangalia uwianisho wa watu wanaoambukizwa Covid-19 wanavyoendelea kupoteza maisha.
Kwa uwianisho, nchi tano ambako kuna wastani mkubwa zaidi wa vifo hivyo, ambako kunalinganikishwa na kwingineko na ama takwimu kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa kwenye wastani wa viwango vya hivi karibuni zaidi duniani chini ya asilimia 5:Chad asilimia 8.5,Algeria asilimia 6.6,Niger asilimia 6.2,Burkina Faso asilimia 5.5, Mali asilimia 5.3.
Lakini Githinji Gitathi, Mkuu wa Amref Health Afrika, NGO ambayo inajihusisha na masuala ya afya, anasema kuwa viwango vya juu vya visa vya ugonjwa huo inawezekana ni kutokana na viashiria vya kuongezeka maambukizi kuliko ambavyo matukio yanavyosajiliwa, na kwamba inawezekana yanakoonekana idadi ziko chini ni sababu ya viwango vidogo vya kupima maambukizi.
Upima idadi ndogo unapofanyika, husababisha visa vipya vichache kugundulika, na hivyo takwimu za vifo hujitokeza kidogo kwa uwiano.
Taratibu tofauti za kuripoti vifo pia huweza kuathiri idadi ya visa vinavyotokana na ugonjwa huo.
Mfano, ambako watumishi wa afya ya jamii na wafanyakazi wengine wanaopambana wanasajili vifo vya Covid-19, kama vile nchini Chad, unaweza kupata viwango vikubwa vya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
KIASI GABI UPIMAJI UNAFANYIKA AFRIKA
Nchi kumi (10) barani ambako upimaji maambukizi ulifanyika zinahusishwa na karibu asilimia 80 ya visa vya ugonjwa huo:
Hizo ni tofauti pana katika viwango vya upimaji, huku Afrika Kusini ikiongoza na Nigeria ikifuata kidogo, kulingana na Our World Data, mraditafiti unaoratibiwa nchini Uingereza, ambao hukusanya taarifa za covid-19.
Julai 4, Afrika Kusini ilifanya vipimo zaidi ya 30 katika watu 1,000, ikilinganishwa na 72 Uingereza na 106 Marekani.Nigeria inafikisha vipimo 0.7 katika watu 1,000, Ghana 10 na Kenya 3.
Inakubalika kufikirisha kuwa, katika baadhi ya nchi za Kiafrika haiwezekani kujua kikamilifu nini haswa kinaendelea kutokana na ukosefu wa taarifa zozote ama taarifa hizo kuwa zenye mapungufu.
“Inabidi tusajili idadi na punje ya chumvi,” anasema Chiedo Nwankwor, Mhadhiri wa Masuala Uhusiano ya Kiafrika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.
Equatorial Guinea iliingia katika mgogoro na WHO baada ya kumshutumu mwakilishi wake nchini humo kuwa alikuwa akiongeza idadi ya visa vya covid-19.Ilizuia taarifa zake kwa muda, lakini sasa imeanza kutoa upya.
Na katika Jimbo la Kano lililoko kaskazini kwa Nigeria, mlipuko usio wa kawaida wa ugonjwa huo uliripotiwa kufikisha idadi ya vifo 1,000 vilivyoripotiwa mwishoni mwa Aprili, mwaka huu, lakini Serikali bado haijathibitisha ni wangapi walipoteza maisha kwa Covid-19.
Taarifa hii ni kwa msaada wa mtandao wa BBC Swahili
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu Ilemela
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika