April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri aiwakilisha Tanzania mkutano wa kimataifa

Na Esther Macha, TimesMajira,Online Mbeya

NAIBU Maziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameiwakilishi Tanzania katika mkutano wa Umoja Mataifa wa Mkataba wa Maji uliohudhuriwa na mataifa zaidi ya 100 kuhusu ushirikiano katika usimamizi wa maji kimataifa.

Mhandisi Mahundi amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha siku tatu wa Mkataba wa Maji wa Kimataifa kilichofanyika kwa njia ya mtandao katika ofisi za Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya.

Kwa mujibu wa naibu waziri huyo maji kimataifa ni yale yanayotumiwa zaidi ya nchi moja mfano. Alitolea mfano maji ya Ziwa Nyasa ambayo yanatumiwa na nchi za Tanzania na Malawi.

“Mkutano umejadili masuala mbalimbali ya maji katika mkutano huo nimepata fursa ya kuhutubia kuhusu maji na amani na kuwa maji ni kichocheo cha ushirikiano na mataifa na pia tunaona maji ni kiungo cha amani, vile vile kulingana na umuhimu wa mkataba huo kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa UN imeonesha nia ya kujiunga katika mkataba huo maji,”amesema Naibu Waziri.

Aidha Mhandisi Mahundi amefafanua kuwa mkataba huo unaendana na sambasamba na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kama alivyosema hivi karibuni wakati akihutubia Umoja wa Mataifa.

Amesema baada ya kushiriki vema katika mkutano huo wameona umuhimu wa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Samia na kuona wanaongeza ushirikiano na nchi mbalimbali.

Naibu Maziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, akishiriki kwa njia ya mtandao me Mkutano wa Umoja Mataifa wa Mkataba wa Maji uliohudhuriwa na mataifa zaidi ya 100 kuhusu ushirikiano katika usimamizi wa maji kimataifa. Mhandisi Mahundi aliiwakilisha Tanzania kwenye mkutano huo.

Akielezea zaidi amesema kuwa baada ya kushiriki vema katika mkutano huo, kumekuwa na umuhimu wa kulinda amani ya nchi na kuchochea uchumi wa taifa.

Amesema pale matumizi ya maji yanapokuwa yanashindikana kuwa katika hali ya makubaliano mazuri wakati fulani inasababisha mapigano,watu kuchafua vyanzo ya maji na kufikia hatua kupoteza shughuli za uvuvi kwa kupoteza mazalia ya samaki.

Hata hivyo, Mhandisi Mahundi amesema baada ya kukamilisha mpango kazi katika kikao cha siku tatu ambacho kimefanyika katika Jiji la Geneva nchini Uswis, kikao hicho kimepokea mpango kazi ambao ulianza mwaka 1919 -2021 na sasa wameanza kuondoka na mpango wa kazi mwingine wa mwaka 2022-2024 na kwamba mkutano mkuu wa kumi utafanyika mwaka, 2024 nchini Slovania.