December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Katibu Mkuu Nishati awasili rasmi ofisini

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba, jijini Dodoma alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha. Felchesmi Mramba, Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) akimkaribisha katika Ofisi za Wizara ya Nishati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dkt. Mataragio amesema, ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi na Taifa kwa ujumla.

“Mimi nashukuru kwa kuteuliwa kutumika katika nafasi hii, na nitaendeleza ushirikiano na watumishi wenzangu, ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake.” Amesema Dkt. Mataragio.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio (kulia) akipokea maua mara baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma tarehe 11 Machi, 2024.