



Na Joyce Kasiki,Dodoma
MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi umewasili nyumbani kwake Area D jijini Dodoma kutoka hospitali ya Benjamini Mkapa ulikokuwa umehifadhiwa.
Lukuvi aliyekuwa Mbunge wa Isimani kupitia Chama cha Mapinduzi amefariki jana 25 Machi 2026 baada ya kupata tatizo mshtuko wa moyo.
Lukuvi anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Idodi mkoani Iringa siku ya Jumanne 31 Machi 2026 ambapo kesho mwili wake utapelekwa Bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya taratibu za ibada na kisha kuelekea jijini Dar Es Salaam ambako 28 Machi utaagwa katika viwanja vya Karimjee.
Aidha kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge 29 Machi 2026,mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Iringa na wananchi wa mkoa watapata nafasi ya kumuaga siku ya Jumatatu 30,Machi na kisha kupelekwa kijiji kwao Idodi kwa ajili ya kuupumzisha mwili wake 31 Machi 2026.Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

More Stories
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni.
Kero za Walimu kutoshughulikiwa kwa wakati chanzo Cha msongo wa mawazo-CWT