
Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeelezwa kuwa ina mchango mkubwa katika kuimarisha uzalishaji wa mazao kupitia huduma za kulinda afya ya mimea na matumizi salama ya viuatilifu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, alipotembelea banda la TPHPA katika Maonesho ya 33 ya Siku ya Wakulima (Nanenane 2026) leo Agosti Mosi,2026 yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, ambapo alipata maelezo kuhusu shughuli na mafanikio ya mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Ndunguru,amesema Mamlaka imeongeza juhudi za kudhibiti baa la panzi, kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu na kuimarisha ulinzi wa afya ya mimea ili kuongeza tija kwa wakulima na kuchangia usalama wa chakula nchini.
Dkt. Nchemba alisisitiza TPHPA kuendelea kuboresha utoaji wa huduma na kuzifikisha kwa wakulima wengi zaidi, akibainisha kuwa hatua hiyo itaongeza uzalishaji wa mazao na kuunga mkono utekelezaji wa kaulimbiu ya Nanenane 2026 inayosema, “Tambua Soko ,ongeza tuja kutekeleza Dira 2050.”


More Stories
Waziri Mkuu Aipongeza TAFICO kwa mafanikio Nanenane
Nchemba aipongeza TPHPA Kwa huduma bora
Mwigulu:TADB ni muhimu kuongeza uzalishaji wa kilimo