May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga atoa maelekezo kwa viongozi wanaosimamia maendeleo Wilayani

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo ikiwemo watendaji wa serikali kuwa hawatomvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo cha kukwamisha maendeleo ikiwemo miradi inayotekelezwa kwa wananchi.

Mwenyekiti Rajab ametoa kauli hiyo wilayani Pangani wakati wa hafla ya kumkaribisha na kumpongeza kufwatia ushindi alioupata wa kiti hicho kwenye uchaguzi mkuu wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ uliofanyika hivi karibuni ambapo kati ya wajumbe 1384 walioshiriki uchaguzi huo takribani 1340 walimchagua kukiongoza chama hicho.

“Tunahitaji tukasukume maendeleo katika mkoa wetu kwenye wilaya mbalimbali kazi ya chama ni kuisimamia serikali wale watendaji wa serikali ambao watakuwa ni wazembe hawatapata nafasi katika mkoa wetu wa Tanga hatutoweza kukubali tunahitaji maendeleo katika maeneo yetu, hatuko tayari kumuonea mtu yule ambaye anaitendea haki nafasi yake”

Amewataka wananchi kuendelea kutoa chagamoto na kero zinazowakabili katika maeneo yao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na kumalizika kabisa.

“Tunajua kuna changamoto nyingi zinazowakumba wananchi zielezeni changamoto zenu na sisi tutumie msukumo wa kisiasa tuweze kutatua changamoto hizi kwa pamoja, sio kukaa kimya mwisho wa siku wananchi wanalalamika” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa uapande wake mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Mohammed Salimu ‘Ratco’ amewaagiza wabunge na madiwqni wote wa mkoa wa Tanga kuwa na utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi ili kujua na kusikiliza kero zinazowakabili pamoja na kuzipatia ufumbuzi.

“Niwaagize madiwani wote wa kata 242 wawe wana utaratibu wa kuweka mikutano ya hadhara na sisi kama viongozi wakuu wa mkoa tutahakikisha tunakwenda kuungana nao kusikiliza matatizo ya wananchi, kama viongozi tuhakikishe tunaisumamia serikali nawaomba sana kuweni na utaratibu huo hii itasaidia kukijenga chama chetu, “alisistiza Ratco.