May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti CCM Mkoa Tanga, awavaa wapinzani wanaobeza miradi mikubwa ya serikali

Na Hadija Bagasha Tanga,

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Rajab Abdulrahman amewavaa wapinzani wanaobeza miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ikiwemo ya umeme, barabara, na reli kwa madai kuwa miradi hiyo inatumia fedha nyingi wakisahau miradi hiyo imekuwa na tija kwa maendeleo ya uchumi wa Nchi.

Mwenyekiti Rajab ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio wa nafasi ya diwani katika kata ya Vibaoni iliyopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga uzinduzi uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

Rajab amesema kuwa chama cha mapinduzi ccm kinaamimi na kuelewa kwamba nchi zilizoendelea zimeendelea kwajili ya uchumi wa viwanda walio nao hivyo miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali imekusudia kuinua uchumi wa Tanzania.

“Ndugu zangu mkisikia nchi za Canada, Brazil, Australia, Marekani, Uingereza au nchi yeyote dunia ukisikia imeendelea ni kwasababu ya viwanda Tanzania tukasema hapana ni lazima na sisi tujemge viwanda vya kutosha katika nchi hii ili tusiwe tunaagiza kila kitu nje ya nchi viwanda vikaanza kujengwa kwa kasi sana wazawa wakaitikia wito wa serikali na wawekezaji kutoka nje ya nchi wakaitika wito viwanda vikajengwa lakini changamoto kubwa ya umeme bado tikaona viwanda havitofanya kazi inavyotakiwa kwasababu umeme uliopo ni mdogo tumelazimika kujenga mradi mkubwa wa umeme pale mto Rufiji, “Alibainisha Mwenyekiti Rajab.

Mwenyekiti Rajab amesema mradi huo mkubwa wa umeme unatekelezwa mto Rufiji umegharimu zaidi ya Trilioni 6 na utakapokamilika utasaidia viwanda vyote viweze kufanya kazi kwa muda masaa 24 na hatimaye kuongeza uchumi wa nchi.

“Pamoja na kufanya haya yote lakini wapinzani bado wanalaumu ndugi zangu hawa watu hawafai ni watu wa kuwakimbia kama ukoma.. wapinzani wa nchi hii ndio waliowahi kutuambia miaka ya nyuma kwamba barabara za lami katika nchi hii zinajengwa kila kona lakini baada ya muda mfupi barabara hizo zinaaribika kwasababu mizigo mizito inasafirishwa kupitia njia ya barabara, “

“Wakasema lau wao wangepewa nchi hii waweze kuiongoza wangetafuta njia mbadala ya kusafirisha mizigo tukawauliza mngefanya nini wakasema sisi tungejenga reli kwajili ya kusafirisha mizigo mizito ipite njia ya reli ili barabara zrtu ziweze kudumu kwa muda mrefu lakini tumefanya hatua hiyo wameanza kulalamika kwwamba ccn wsmechukua mahela chungu nzima wameweka kwenye reli jaman watu waongo hawa, “alisema Rajab.

Mwenyekiti Rajab amesema kuwa wanapowaambia wananchi na watanzania kwa ujumla kwamba kuna kila sababu ya kuchagua chama cha mapinduzi ccm huwa wanamaanisha kwamba lengo lao kubwa ni kuwaletea maendeleo.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Rajab amewaasa wakazi wa Handeni kuchangamkia fursa kulima kwa bidii zao la mahindi ambalo limekuwa na mtokeo makubwa visiwani Zanzibar.

“Sisi hapa Handeni tuchangamkeni tupo jirani na Pangani na Pangani pale ndugu zangu tuko karibu na Zanzibar nyinyi wana Handeni huku mnazalisha sana mahindi watu wa Zanzibar wanapenda sana kula ugali unaoagizwa kutoka Tanga kwahiyo mnayo fursa kubwa ya kulima kwa bidii kwasababu soko Zanzibar lipo na njia pekee ya kupitia ni Pangani ili muweze kukuza kipato chenu.

Mbunge wa jimbo la Handeni Vijijini John Salu amesema watanzania wana kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na namna ambavyo amekuwa akiwaoetea watanzania maendeleo.

Awali akizungumzia mradi wa maji unaotekelezwa Wilayani humo Mbunge Salu amesema kuwa Rais amewapelekea mradi mkubwa wa maji wa miji 28 ambapo katika mradi huo litajengwa tanki la lita milioni 2 juu ya mlima wa Handeni na kutiririsha maji kwenye kils kona ya Handeni.

“Mama yetu huyu pamoja na kutusaidia fedha kwenye miradi mbalimbali lakini bado unakuja mradi mkubwa wa kuikoa Handeni kabisa nabaada ya muda Handeni tutakuwa tunazungumzia changamoto nyingine na sio maji, “alisema Mbunge Salu.

Mbunge Salu amesema Rais amewakubalia ombi lao la kutengeneza barabara ya Handeni, Kwediboma, Kibirashi mpaka Singida na awamu ya kwanza ya kilomita 20 mkandarasi yuko saiti anaendelea na ujenzi huku amwamu ya pili ya kilimita 30 imeshatiwa saini ili ifike Kwediboma, na awamu ya tatu ya kutoka Kwediboma kwends Singida ipo kwenye manunuzi ambapo mradi huo ukikamilika uchumi wa Handeni utafunguka kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo katika ufunguzi huo wa kampeni aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Handeni Halfan Mwanabonde amemkabidhi Mwenyekiti Rajab kadi yake ya CUF na kutimkia chama cha mapinduzi ccm huku akiahidi kwenda kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuwaletea maendeleo watanzania.

Katika ufunguzi wa Kampeni hizo wananchi wa kata ya Vibaoni wameaswa kumchagua Mery Mntambo ambaye ni mgombea udiwani wa kata hiyo ili aweze kushirikiana na viongozi wa serikali kupitia chama cha mapinduzi kuwaletea wana Handeni maendeleo.

Uchaguzi mdogo wa nafasi hizo za udiwani unatarajiwa kufanyika desemva 17 mwaka huu.