Judith Ferdinand,TimesMajira Online, MwanzaMtendaji wa Kata ya Ilemela, wilayani Ilemela mkoani Mwanza ametakiwa kutumia pikipiki iliyotolewa na serikali kwa lengo lililokusudiwa.
Pikipiki hiyo ni miongoni mwa pikipiki 916 zilizotolewa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watendaji wa Kata nchini ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ni moja ya wanufaika.
Hayo yamebainishwa Machi 7, mwaka huu na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga,wakati akimkabidhi pikipiki hiyo Mtendaji huyo wa Kata ya Ilemela ambapo halmashauri hiyo imepata pikipiki moja kati ya zilizotolewa na Rais.
Mulunga, ameeleza kuwa Mtendaji huyo anapaswa kutumia pikipiki hiyo kwa lengo lililokusudiwa pamoja na kuhakikisha anatekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Ilemela Nkuba Charles, ameeleza kuwa pikipiki hiyo itamrahisishia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Hivyo kuboresha utendaji kazi katika kata yake ya Ilemela pamoja na urahisi wa kuhudumia wananchi huku akiahidi utendaji uliotukuka kwa kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanapata huduma iliyo bora.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu