MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mbarali kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na Diwani wa kata ya Chimala mwaka 2015 hadi 2020 ,Francis Mtega amechukua fomu ya kuwania Jimbo hilo katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Mtega amekabidhiwa fomu hiyo na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbarali ,Kivuma Msangi .
Mgombea huyo aliongozana na Mbunge aliyemaliza muda wake, Haroon Pilmohamed Mullar, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, walioteuliwa kugombea Udiwani kwenye kata kupitia Chama Cha Mapinduzi pamoja na wale waliokuwa wametia nia kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi katika nafasi ya Ubunge.
More Stories
GreenFaith yatoa mapendekezo yake mkutano wa mission 300 kwa Wakuu wa nchi,Serikali za Afrika
Mwenyekiti UVCCM ataka wakandarasi kuwa na weledi ujenzi wa miradi
RC Mrindoko aweka kambi Njombe kujifunza kutomeza udumavu wa watoto