May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Magufuli ambaye utafiti wa maoni shirikishi kutoka kwa wananchi wamemtaja kuwa ndiye chaguo lao kutokana na kazi kubwa aliyoifanya tangu 2015 hadi 2020 katika Serikali ya Awamu ya Tano. (Picha na Maktaba).

Mshike mshike majimboni, Magufuli, makada wang’ara Mtwara Mjini, Iringa Mjini, Arusha Mjini, Hai,Ubungo, Kigoma Mjini, Tarime, Mbeya Mjini

Na Waandishi Wetu, TimesMajira Online, Mikoani

UTAFITI wa maoni shirikishi kutoka kwa wananchi umebainisha kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri katika ngome za upinzani iwapo watapelekewa watu ambao ni chaguo lao,sahihi na wenye uwezo wa kwenda kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekeleza ilani kwa mafanikio makubwa kama ilivyokuwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.

Hayo ni matokeo ya maoni shirikishi baina ya wananchi wa majimbo zaidi ya 10 ambao walianza kuhojiwa na wawakilishi wa TimesMajira Online kwa nyakati tofauti tangu Januari Mosi, mwaka huu hadi mwezi huu.

Kwa nyakati tofauti wananchi walieleza kuwa,bado wana imani kubwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dkt.John Magufuli kutokana na misimamo yake ya kukemea rushwa na kuchukua hatua mara moja kwa wahusika ambao wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na vitendo hivyo.

Pia walisema, katika kipindi cha miaka mitano chini ya Rais Dkt.John Magufuli wameshuhudia mafanikio makubwa yakiwemo mageuzi ya kihistoria katika sekta za afya, elimu, uchumi,miundombinu, usafiri wa anga, majini na nchi kavu na mengine mengi, hivyo wana kila sababu ya kupata timu ambayo ni ya watu wachapa kazi na wazalendo.

MTWARA MJINI

Majimbo hayo ni pamoja na Mtwara Mjini ambalo Dkt.John Magufuli anatajwa kwa asilimia 95 ya kukubalika kulingana na maoni shirikishi ya wananchi huku Hassan Mtenga akitajwa kwa asilimia 87.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hassan Mtenga ambaye wananchi katika Jimbo la Mtwara Mjini wamemtaja zaidi kupitia utafiti shirikishi wa wananchi.

Wengine ni Hasnen Murji ambaye ametajwa kwa asilimia 31, Edward Laurent Kapwapwa kwa asilimia 20, Husein Said Kasugulu kwa asilimia 38, Said Swala kwa asilimia 7,Musa Chimae asilimia 29, Charles Mkilawa kwa asilimia 20, Siraji Nalikame kwa asilimia 21, Salum Burian kwa asilimia 16, Andrew Kifuwa kwa asilimia 14, Shahid Mustakim Murji asilimia 17, Abdul Swamad asilimia 14, Tito Shengena kwa asilimia 7.

Aidha, Saidi Kiwamba anatajwa kwa asilimia 6, Godfrey Mwanchisy asilimia 5, Salum Mfaume Salum asilimia 4, Clemence Cleninus 18, Amida Mwarabu asilimia 19, Baltazari Komba asilimia 13,Yusuph Achiula asilimia 8.

Mbunge aliyemaliza muda wake Maftah Abdallah Nachuma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) anatajwa kwa asilimia 31 huku nafasi ya urais kwa upande wa upinzani wakitajwa kwa asilimia 3.

HAI

Kwa upande wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Dkt.John Magufuli ametajwa kwa asilimia 88 huku nafasi ya ubunge Fuya Godwin Kimbita akitajwa kwa asilimia 61, Martin Munis asilimia 18, Keshisha Mafuwe asilimia 16, Jery Muro asilimia 36, Evod Njau asilimia 15 na Joseph Msele asilimia 13.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Fuya Godwin Kimbita ambaye ametajwa zaidi katika utafiti shirikishi wa maoni ya wananchi katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

Mbunge aliyemaliza nafasi yake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anatajwa kwa asilimia 42 huku nafasi ya urais vyama vya upinzani wakitajwa kwa asilimia 10 na asilimia 2 walionekana kutoegemea upande wowote.

Aidha, nafasi ya urais Jimbo la Iringa Mjini, Rais Dkt.John Magufuli anatajwa kwa asilimia 83, upinzani nafasi ya urais asilimia 12 na asilimia 5 hawakutaja.

KILOLO

Jimbo la Kilolo mkoani Iringa katika nafasi ya ubunge, Festo John Kipate ametajwa kwa asilimia 69, Justine Nyamoga asilimia 44, Askofu Mdegela asilimia 42, Bryan Kikoti asilimia 43, Venance Mwamoto asilimia 41.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Festo John Kipate ambaye ametajwa zaidi katika utafiti wa maoni shirikishi ya wananchi katika Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.

Wengine ni Danford Mbilinyi asilimia 39, Cherestino Mafuga asilimia 37, Ashiraf Chusi asilimia 35,Mugabe Kiongozo asilimia 32, Melick Luvinga asilimia 30, Mwalimu Mdegela asilimia 27, Yangalay Mkulago asilimia 21. Huku kwa upande wa nafasi ya urais, Dkt. John Magufuli akitajwa kwa asilimia 95, upinzani asilimia 2 na asilimia 3 hawakutaja upande wowote.

IRINGA MJINI

Kwa nafasi ya ubunge Iringa Mjini, Nguvu Chengula anatajwa kwa asilimia 52,Albert Chalamila asilimia 41, Joseph Said Mgongolwa kwa asilimia 60, Jesca Msambatavangu kwa asilimia 41,

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Mgongolwa ambaye ametajwa zaidi katika Jimbo la Iringa Mjini kupitia utafiti wa maoni shirikishi kwa wananchi.

Peter Mwanilwa asilimia 21,Bavan Mwakiambiki asilimia 20,Joseph Liyatuu kwa asilimia 17,Richard Kasesela kwa asilimia 49, Kenan Kiongosi kwa asilimia 32. Mbunge aliyemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa anatajwa kwa asilimia 39.

MBEYA MJINI

Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt.Tulia Akson Mwansasu anatajwa kwa asilimia 67, Ndele Maselela kwa asilimia 45,Charles Mwakipesile kwa asilimia 48, Mashaka Mbugi kwa asilimia 30, James John Siluamba kwa asilimia 28, Brown Mwakalikamo kwa asilimia 25 na Amani Kajuna kwa asilimia 21.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Tulia Ackson ambaye ametajwa zaidi katika utafiti shirikishi wa maoni ya wananchi katika Jimbo la Mbeya Mjini mkoani Mbeya.

Nafasi ya urais Mbeya Mjini, Rais Magufuli anatajwa kwa asilimia 81 kwa upande wa upinzani wanatajwa kwa asilimia 16 huku asilimia 3 wakidai bado wanatafakari, huku Mbunge aliyemaliza muda wake,Joseph Mbilinyi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitajwa kwa asilimia 41.

ARUSHA MJINI

Utafiti huo wa maoni shirikishi kutoka katika Jimbo la Arusha Mjini, wananchi walimtaja Mrisho Gambo kwa asilimia 50, Monaban Molel kwa asilimia 50, Justine Nyari Nyari kwa asilimia 35, Laizer Molel kwa asilimia 32, Albert Msando kwa asilimia 31, Victor Molel kwa asilimia 29, Emmanuel Lusenga kwa asilimia 27.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Gambo ambaye katika Jimbo la Arusha Mjini amegongana katika asilimia na Kada mwingine Monaban Mollel (hayupo pichanai).

Mbunge aliyemaliza muda wake, Godbless Lema alitajwa kwa asilimia 50 huku nafasi ya urais, Rais Dkt.John Magufuli akitajwa kwa asilimia 85, upinzani kwa nafasi ya urais wanatajwa kwa asilimia 8 huku asilimia 7 wakidai bado wanatafakari.

TARIME VIJIJINI

Kwa upande wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Gimunt anatajwa kwa asilimia 43, Mwita Waitara asilimia 20,Nicodemus Kelaryo asilimia 25,Nyerere Mwera asilimia 10, Christopher Kangoye asilimia 27,Eliakimu Maswi kwa asilimia 50,Bwire Alliance asilimia 30, Manchare Heche asilimia 34, Dkt.Steven Yusuph asilimia 30, Dkt.Paul Mwikwabe kwa asilimia 29. Mbunge aliyemaliza muda wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche anatajwa kwa asilimia 40.

Aidha, nafasi ya urais, Dkt.John Magufuli anatajwa kwa asilimia 89 huku asilimia 10 wakitajwa wapinzani na asilimia moja ilitaja pande zote.

TARIME MJINI

Kwa upande wa Jimbo la Tarime Mjini, Julius Mtatiro anatajwa kwa asilimia 39, Jackson Kangoye anatajwa kwa asilimia 40,Gerald Mandevu kwa asilimia 40,Michael Kembaki kwa asilimia 42,Deo Meck kwa asilimia 25,Kisyeri Chambiri kwa asilimia 30. Mbunge aliyemaliza muda wake, Esther Matiko kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatajwa kwa asilimia 40. Nafasi ya urais, Dkt.John Magufuli ametajwa kwa asilimia 93 huku wapinzani wakitajwa kwa asilimia 5, na asilimia 2 walitaja pande zote.

UBUNGO

Wakati huo huo, katika Jimbo la Ubungo,Mhandis Burton Kihaka anatajwa kwa asilimia 68, Dastun Mapunda kwa asilimia 24,Edwin Mrema kwa asilimia 36, Juma Pangalugome kwa asilimia 21.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mhandisi Burton Lumuliko Kihaka ambaye kupitia utafiti wa maoni shirikishi ya wananchi katika Jimbo la Ubungo ametajwa zaidi.

Wengine ni Calist Lyimo kwa asilimia 38, Kitila Mkumbo kwa asilimia 32, Hawa Ng’umbi kwa asilimia, Issa Mituro kwa asilimia 17, Fatuma Msofe kwa asilimia 15, Atiki Swalehe kwa asilimia 12, Mwamtumu Mgonja kwa asilimia 23. Mbunge aliyemaliza muda wake, Said Kubenea anatajwa kwa asilimia 35 huku kwa upande wa urais, Dkt.John Magufuli akitajwa kwa asilimia 97, upinzani upande wa urais wanatajwa kwa asilimia 3.

KIGOMA MJINI

Jimbo la Kigoma Mjini, James Nyabakari ametajwa kwa asilimia 71, Kilumbe Ng’enda kwa asilimia 45, Adam Idd Mgoye asilimia 38, Hamad Sovu asilimia 36, Baruan Muhuza asilimia 34, Jacob Ruvilo asilimia 31, Peter Msanjila asilimia 30, Justin Rukiga asilimia 21, Maulid Kikondo asilimia 17, Juma Kihenge asilimia 7, Shaban Shaban asilimia 5, Shaban Kapeche asilimia 4, David Dyoya asilimia 3, Wilson Mwambe asilimia 2, Zuberi Mabie asilimia 1.

Mbunge aliyemaliza muda wake, Zitto Kabwe ametajwa kwa asilimia 49 huku nafasi ya urais, Dkt.John Magufuli anatajwa kwa asilimia 88 na wapinzani wakitajwa kwa asilimia 11 na asilimia moja ilitaja pande zote.

Hata hivyo, kupitia utafiti huu wa maoni shirikishi ya wananchi, majimbo ya Mtwara Mjini, Hai, Ubungo na Kigoma Mjini nafasi ya ubunge wenye asilimia nyingi walionekana kutajwa mara nyingi zaidi kila eneo la mahojiano na wananchi.