May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MNMA wajivunia kuendeleza amani, umoja Kitaifa

Na Rose Itono
UONGOZI wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA )umesema maarifa Bora na uendelezaji wa amani na Umoja Kitaifa unaosimamiwa chuoni hapo umechangia kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi kutoka 14,238 mwaka 2022/23 hadi kufikia 17,200 mwaka 2023/24

Akizungumza kwenye kusanyiko la Wahitinu waliosoma chuoni hapo Dar es Salaam jana Mkuu wa Chuo Cha MNMA Prof. Shadrack Mwakalila amesema dira ya chuo ni kuwa kitovu cha utoaji maarifa bora, elimu mafunzo na kuendeleza amani na Umoja wa Kitaifa

Amesema ongezeko la wanafunzi ni ishara kuwa, wanafunzi, wazazi na walezi wanaimani na chuo na mategemeo makubwa ya kupata Wahitimu walioelimika na wenye maarifa na ujuzi wa kuchangia haraka maendeleo ya taifa

Prof Mwakalila amesema chuo kitaendelea kuwa kitovu cha utoaji wa maarifa bora kwa kutoa elimu na kuendeleza amani na Umoja wa kitaifa

” Chuo hakitaacha kutoa mafunzo katika fani mbalimbali za kitaaluma, kutoa mafunzo ya uongozi, maadili na utawala bora,” alisema Prof Mwakalila na kuongeza kuwa pia hakitaacha kufanya tafiti zenye majibu yanayoweza kutatua changamoto za kijamii

Aidha amesema pia chuo hakitaacha kutoa mafunzo yankujiebdeleza ka wanafunzi watakaosoma MNMA Ili kuwajenga katika misingi ya kujitegemea

Ameongeza kuwa MNMA itazifanyia kazi changamoto zote zilizowasilishwa na Reiner Wigira ambaye ni Mjumbe wa kusanyiko hilo kwa niaba wa Katibu wake.

Wigira amesema Kamati Tendaji ya Kusanyiko la Wahitinu waliomaliza MNMA inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na mtu au ofisi inayojishughulisha pekee na kusanyiko la Wahitinu ikiwemo kusajili na kutunza taarifa za wahitimu

Amesemawajumbe kushindwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya Kusanyiko kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo

Wamependekeza kutokana na ongezeko kubwa la Wahitinu chuo kianzushe rasmi ofisi inayoshughulika na masuala ya Kusanyiko Ili kuboresha utendaji kazi wa Shughuli zote za kusanyiko sambamba na kuweka utaratibu mzuri wa Wahitinu kulipa ada za uanachama fedha ambazo zitasaidia chuo kwenye tafiti na ufadhili katika bunifu zinazoibuliwa