May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TOMA yazindua mpango mkakati wa miaka mitano

Na Penina Malundo, timesmajira

TAASISI ya Tanzania Online Media Alliance (TOMA) imezindua Mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2024 hadi 2025.

Akizindua Mpango huo jana Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa UTPC, Kenneth Simbaya amewataka viongozi kuwa na nidhamu ili kuweza kufikia malengo.

“Mipango mikakati mingi inafeli kwasababu ya kutokuisimamia vizuri…ushauri wangu msisahau malengo yenu kwani safari ndo kwanza mmeianza. Fanyeni kazi kwa bidii, pambaneni ukilinganisha na mazingira ya ushindani katika soko mnalokwenda kulifanyia kazi.

“Hata barabara tunazopita usipofuata kanuni unapata ajali, na mpango mkakati utekelezaji wake unahitajika nidhamu ya kazi. Hakikisheni TOMA inawaunganisha pamoja waandishi wa habari za mtandaoni,”amesema

Amesema ni vema kuhakikisha mpango mkakati unaendana na miundombinu iliyopo ili kuweza kuleta maendeleo.

Amesema Taasisi hiyo inapaswa kufanya uwepo wa mitandao inakuwa ni manufaa ya umma.

“Mitandao ina mambo mengi, ina faida na hasara Sasa TOMA lazima mhakikishe mnaitumia kwa manufaa ya umma” amesema.

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Salome Kitomari amesema TOMA inaundwa na wanahabari zaidi ya 200 wanaopandisha maudhui mtandaoni nchi nzima.

“Tumeandaa mpango mkakati huu kwa kusaidiwa na Freedom House, tunawashukuru kwa msaada huo mkubwa kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni mnatuleta pamoja. Ndani ya mpango mkakati huu tutahakikisha mambo yote yapo ikiwemo kuwawezesha Wanahabari kuendana na teknolojia,” amesema Kitomar