Na Stephen Noel – Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ,Sophia Kizigo amesema hajaridhishwa na ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo hali aliyosema inatishia uendelevu wa miradi ya maendeleo inayoibuliwa na wananchi ngazi za vijiji na kata.
Kizigo ameyasema halmashauri hiyo ikiwa katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 wamefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 41.2% kitu alichosema kinaweza kutishia halmashauri kushidwa kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato katika halmasahauri hiyo.
Aidha akianisha sababu za halmashauri hiyo kuendelea kusuasua katika ukusanyaji ni usimamizi mbovu wa mapato, lakini uzembe wa kusimamia mapato na baadhi ya vyanzo kama madini ya ujenzi ikiwemo vifusi vya kujengea barabara na miundo mbinu mingine na kuwatumia watu ambao si wataalamu wa uchumi katika kukusanya mapato.
Amesema ili kufanikisha hilo lazima watendaji wa kata vijiji pamoja na madiwani washirikiane katika kusimamia na vyanzo vya mapato na kuviwasilisha kwa mamalaka husika.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa ambae amebobea katika usimamizi wa fedha, George Nathan Malima amedai kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanya na mawakala wa ukusanyaji mapato ambapo wakikusanya hawawasilishi fedha benki hiyo kukaa na fedha majumbani kitu alichokisema kuwa kinaweza kikawa kinachangia kuto kufikia lengo.
‘’Kiukweli ni uzembe wa hali ya juu pesa inakusanywa haipelekwi benki lakini pia kunapesa zinatumika pesa mbichi bila kufuata utaratibu kwa maelekezo ya wakuu wa idarakitu ambacho si kizuri sana katika uhasibu’’ Ameongea.
Diwani wa kata ya berege ambae ni mjumbe wa kamati ya uchumi mipango na fedha ,Baraka Habari amesema mapato mengi ya halmasahauri hiyo yanavuja sana kwa kukosa usimamizi madhubutu.
“Kwa mafano si kwamba mapato hayakusanyi hapana mapato yanakausanaya ila mawakala na watendeji wa kata hawapeleki fedha hizo Benki wa wakati na mapato mengi yanavuja mfano tumefanya ambushi ya mapato katika mnada wa Chipogolo ambapo timu pekee ilikuwa inawasilisha shilingi million 4 lakin baada ya madiwani kuungana na madiwani wameweza kukusanya hadi million sita ndipo tulipobaini kuwa mapato ya halamasahauri yanaliwa kwa kukosa usimamizi mathubuti” ameongea.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi