Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imepongezwa kwa kuendelea kuwajali wanawake katika shughuli mbalimbali ambazo wamekuwa wakifanya katika kijiinua kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Paradise miision Pre&Primary School ,Ndele Mwaselela wakati akizungumza na wanawake wajasiliamali(Familia moja) kutoka kata mbalimbali Jijini hapa.
“Kupitia hadhara hii naomba nipongeze serikali ya mkoa chini ya mkuu wa mkoa wa mbeya Juma homera anafanya kazi kubwa ya kuwalea wanawake ,kwani nimeambiwa kila mnapotaka kufanya shughuli zenu mnapewa ukumbi bure pia ni mara chache sana kukuta baadhi ya mikoa wakifanya kitu kama hichi lakini mbeya imewezekana “amesema Mkurugenzi huyo .
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua