April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkumbo ataka mazingira mazuri ya biashara kwa nchi za A/Mashariki

Na Mwandishi wetu, Timesmajira online

SERIKALI imesema kuwa upo umuhimu wa Jumuiya za Afrika Mashariki kwa ujumla kuendelea kuwapa wafanyabiashara mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Hayo yamesemwa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo ametoa kauli hiyo mara baada ya kizindua maonesho ya wiki ya Viwanda ya Afrika Mashariki ambapo mabalaza ya Biashara na Kilimo kutoka Tanzania, Kenya, Burundi pamoja na Nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki yamekutanishwa kwa lengo la kujadili maendeleo ya sekta ya Viwanda na Biashara pamoja na kukuza Ushirikiano baina ya nchi hizo.

Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es salaam Jana mara baada ya kuzindua wiki ya Maonyesho Viwanda ya Afrika Mashariki ambayo yanaendelea katika ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere Mkoani Dar es Salaam.

Amesema kongamano hilo ni mwendelezo wa maelekezo yaliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu Mei 4 hadi 5 katika ziara yake hivi karibuni nchini Kenya.

“Tunataka tuone biashara kati ya nchi zetu zinakua kwa kiasi kikubwa, tunashukuru baada ya kile kikao na mikutano yote iliyofanyika tumeanza kuona matunda “amesema Profesa Mkumbo

Akitolea mfano Profesa Mkumbo amesema biashara kati ya Tanzania na Kenya katika miezi mitatu iliyopita imeongezeka mara sita kwa kwenda Kenya na kutoka kwenda Tanzania .

“Haya ndo mambo ambayo tulikuwa tukiyataka tunataka kukuza biashara ndani ya Afrika Mashariki “amesisitiza Profesa Mkumbo.

Hata hivyo amesema wafanyabiashara wa Afrika Mashariki ni lazima wafanye biashara zao kwa kuzingatia ukweli na maadili kwani ndio msingi mzuri wa Biashara na kuaminiana kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.

Alibainisha kuwa uaminifu baina ya nchi ya Tanzania na Kenya ni mkubwa zaidi na licha ya kujitikeza kidogo chagamoto na kueleza kuwa nchi hizo kwa sasa zimekuwa ndugu .

“Kenya Tanzania undugu wetu unazidi kuimarika ni mzuri na wananchi wanafurahi…ukitaka kuona wananchi wanafurahia nenda Namanga, Tanga mpakani utaona wananchi wetu wanavyoshirikiana”amesema Profesa Mkumbo

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Nchi ya Kenya, David Osiany amesema hakuna Biashara yoyote inayoweza kufanyika pasipo kuaminiana na kueleza kuwa kinachokuza urafiki baina ya nchi hizo nikutokana na uwepo wa uaminifu na kuaminiana.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Jamhuri ya Kenya ,David Osiany akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho hayo yanayoendelea katika ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere

“Nchi ya Tanzania na Kenya tumekuwa tukiishi kwa uaminifu na hatimaye kufikia hatua hii, Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kwa kuchukua jukumu na kuhakikisha biashara kazi ya nchi hizi zinaendelea na kupanuka”

Na kuongeza kuwa” Sisi kama nchi ya Kenya tutahakikisha urafiki huu tulionao baina ya Tanzania na Kenya unakuzwa vizuri na kutolea mfano “Tangu Rais Samia Hassan Suluhu aje nchini Kenya kule Namanga mwenendo wa biashara na bidhaa baina ya nchi hizo mbili umepanda mara sita katika miezi minne tu”amesema Osiany

Naye Raisi wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Paul Koyi amesema lengo la maonesho hayo ni kujadili na kuona fursa za Biashara sambamba na kuwaweka wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya pamoja na Afrika Mashariki Kama njia ya kuhitimisha maelekezo yaliyolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu aliyiyatoa Nchini Kenya hivj karibuni.

Amesema katika maonesho hayo zimeshiriki nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Kongo, Botswana pamoja na Namibia.