May 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mjumbe wa NEC Hamoud Jumaa amewaasa vijana wasipigane vita katika uongozi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mjumbe wa Halmashauri Kuu(CCM) Taifa MNEC Hamoud Jumaa, amewasa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) Wilaya ya Ilala kufanya kazi za chama na Jumuiya kwa ajili ya kujenga chama na Serikali wasipigane vita katika nafasi za uongozi kwani ukimpiga vita mwezako na wewe utapigwa vita

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ccm Taifa Hamuod Abuu Jumaa, alisema hayo Wilayani Ilala katika Baraza la Jumuiya ya Vijana UVCCM Wilaya ya Ilala ambapo alikuwa Mgeni rasmi .

“Naomba vijana wa Wilaya ya Ilala mfanye kazi za jumuiya na chama na Kila mtu kujua umuhimu wa majukumu yake kwa kutenda haki makundi sio mazuri hayasaidii popote Jumaa Mizungu ni Mwenyekiti wa miaka Mitano,Said Sidde ni Mwenyekiti wa CCM wa Miaka Mitano makundi hayatasaidia chochote katika chama ukimpiga vita mwezako katika nafasi ya Uongozi na wewe utapigwa vita katika nafasi yako ” alisema Jumaa.

Aliwataka kila mmoja kuwa mwema kwa mwezake CCM sasa tujipange vijana Wana nafasi kubwa ndani ya chama watoke watumie fursa kugombea nafasi mbalimbali wachaguliwe viongozi wanaokubalika vizuri .

Aliwataka UVCCM Wilaya ya Ilala kuwa na Mikakati ya kuakikisha CCM Ilala inashika Dola katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na madiwani .

Aidha alitumia nafasi hiyo kuelezea mmomonyoko wa maadili aliwaasa vijana wasitumike katika matendo ambayo yanaenda kinyume na utamaduni wa nchi yetu aliwataka Vijana kupambana katika kuisaidia Serikali .

Aliwataka Vijana kuangalia fursa na kuzisemea katika utekekezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi katika KAZI zinazofanywa na Dkt Samia Suluhu Hasaan .

“Ndani ya Umoja wa Vijana kuna chimbuko la watu muhimu katika serikali hii ambao wengine Wakuu wa mikoa Wakuu wa Wilaya na Makatibu wametokea umoja wa Vijana hivyo watumie nafasi hizo kwa kufanya kazi kwa weledi katika kuisaidia serikali .

Aliwataka Vijana kutumia mitandao vizuri kuisemea serikali kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa Rais wa mfano kufungua nchi Sekta ya utalii kwa ajili ya kujenga uchumi wa nchi .