Na Esther Macha,Timesmajira,Timesmajira,Online,Chunya
NAIBU waziri wa maji na Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Mbeya,Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi mtungi wa kuchakata mawe ya dhahabu (Karasha) wenye thamani Mil.9.5 kwa umoja wa wanawake Chunya ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akikabidhi Karasha hilo leo Mhandisi Mahundi amesema kuwa mradi aliokabidhi kwa wanawake ni moja ya ahadi zake kwa kila wilaya kuwawezesha kuwa na miradi yao ambayo itakuwa kitega uchumi wao .
“Nilitoa ahadi kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya kuzipatia miradi yenye thamani ya shilingi mil.20 lakini kwa kuanzia nimeona nianze na Chunya ambao wao walichagua mradi wa karasha wenye thamani ya shilingi mil.9.5 huu ni mwanzo tu tunaanza ,ndugu zangu wanawake karasha hili lisikae bure na kushika kutu nataka liende eneo la kazi lifanye kazi “amesema Mhandisi mahundi.
Hata hivyo mhandisi Mahundi amesema kuwa mpango wake wa maendeleo kwa wanawake kwa kila wilaya ni kuhakikisha unatekelezeka kama alivyotoa ahadi zake kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.
“Kwa maana yangu nimetoa ahadi kwa vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wangu na zaidi na huu ni mwanzo tuu nataka ndani mwaka mmoja wa Ubunge wangu nitekeleze vyote kwani hapa nina nina miaka mitano ya kuwahudumia na ninachojua wanawake tumejaliwa kupenda maendeleo zaidi sio mtu wa kutuletea maneno maneno “amesema Mhandisi Mahundi .
Akielezea zaidi Naibu Waziri huyo amesema kuwa wilaya ya chunya imejaliwa kwa kuwa na madini ya dhahabu ya kutosha hivyo anaamini ndani ya mwaka mmoja wanawake wa wilaya hiyo watakuwa vizuri kiuchumi kupitia mradi huo wa karasha .
Akishukuru kwa niaba ya umoja wa wanawake Katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya ,Zaitun Sembo amesema kuwa wilaya ya chunya walichagua mradi wa karasha ambalo litakuwa linasaga mawe ambalo ndilo Mbunge amekabidhi kwa wanawake wa wilaya ya chunya.
Aidha Sembo amesema mhandisi Mahunfi amekuwa msaada mlubwa kwa wanawake na kuhakikisha kuwa kola wilaya wanapatiwa mradi wa ujasiliamali ili waweze kijikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Chunya ,Simon Mayeka aliutaka uongozi wa umoja wa wanawake wilayani humo kutafuta eneo ambalo halina migogoro ambalo wataweka mtungi huo wa kusaga mawe (karasha)ili kusonga mbele zaidi .
“Ndugu zangu huu mradi naomba uwe endelevu zaidi ya hapa mmepewa msaada na Mbunge wenu wa vitimaalum mkoa wa Mbeya ambaye pia Naibu Waziri wa maji Mhandisi Mahundi huu ni mwanzo wa mafanikio naombeni lizae lingine zaidi ya hapa ili muweze kumpa moyo Mbunge wenu “amesema Mkuu huyo wa wilaya .
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote