April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi awapa  tabasamu kwa umoja wanawake Chunya akabidhi mtungi wa kuchakata mawe wa sh, mil.9.5

Na Esther Macha,Timesmajira,Timesmajira,Online,Chunya

NAIBU waziri wa maji na Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Mbeya,Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi mtungi wa kuchakata mawe ya  dhahabu (Karasha) wenye thamani Mil.9.5 kwa umoja wa wanawake Chunya ili waweze  kujikwamua kiuchumi.

Akikabidhi Karasha  hilo  leo Mhandisi Mahundi amesema  kuwa mradi aliokabidhi kwa wanawake ni moja ya ahadi zake kwa kila wilaya kuwawezesha kuwa na miradi yao  ambayo itakuwa kitega uchumi wao .

“Nilitoa ahadi kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya  kuzipatia miradi yenye thamani ya shilingi mil.20 lakini kwa kuanzia nimeona nianze na Chunya ambao wao walichagua mradi wa karasha wenye thamani ya shilingi mil.9.5  huu ni mwanzo tu tunaanza ,ndugu zangu wanawake karasha hili lisikae bure  na kushika kutu nataka liende eneo la kazi lifanye kazi “amesema Mhandisi mahundi.

Hata hivyo mhandisi Mahundi amesema kuwa  mpango wake wa maendeleo  kwa wanawake  kwa kila wilaya ni kuhakikisha unatekelezeka  kama alivyotoa ahadi zake kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya.

“Kwa maana yangu nimetoa ahadi kwa vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wangu  na zaidi  na huu ni mwanzo tuu nataka ndani  mwaka mmoja wa Ubunge wangu nitekeleze vyote  kwani hapa nina nina miaka mitano  ya kuwahudumia na ninachojua wanawake tumejaliwa kupenda maendeleo  zaidi sio mtu wa kutuletea maneno maneno “amesema Mhandisi Mahundi .

Akielezea zaidi Naibu Waziri huyo amesema kuwa wilaya ya chunya imejaliwa kwa kuwa na madini ya dhahabu ya kutosha hivyo anaamini ndani ya mwaka mmoja wanawake wa wilaya hiyo watakuwa vizuri kiuchumi kupitia mradi huo wa karasha .

Akishukuru  kwa niaba ya umoja wa wanawake Katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya ,Zaitun  Sembo amesema kuwa wilaya ya chunya walichagua mradi wa karasha ambalo litakuwa linasaga mawe ambalo ndilo  Mbunge amekabidhi kwa wanawake wa wilaya ya chunya.

Aidha Sembo amesema mhandisi Mahunfi amekuwa msaada mlubwa kwa wanawake na kuhakikisha kuwa kola wilaya wanapatiwa mradi wa ujasiliamali ili waweze kijikwamua kiuchumi.

Akizungumza katika mkutano  huo Mkuu wa wilaya ya Chunya ,Simon Mayeka aliutaka uongozi wa umoja wa wanawake wilayani humo kutafuta eneo ambalo halina migogoro ambalo wataweka mtungi huo wa kusaga mawe (karasha)ili kusonga mbele zaidi . 

“Ndugu zangu huu mradi naomba uwe endelevu  zaidi ya hapa mmepewa msaada na Mbunge wenu wa vitimaalum mkoa wa Mbeya ambaye pia Naibu Waziri wa maji Mhandisi Mahundi huu ni mwanzo wa mafanikio  naombeni lizae lingine zaidi ya hapa ili muweze kumpa moyo Mbunge wenu “amesema Mkuu huyo wa wilaya .