May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meneja NIC awakaribisha wananchi kutembelea Banda lao kwenye monyesho ya madini

Na David Johntimesmajira online Gaita

MENEJA wa NIC Insurance Kanda ya ziwa Stella Marwa amewashauri wa chimbaji wa madini kote nchini kukata bima ambayo itawasaidia katika shughuli zao la Kila siku hususani kwenye sekta ya madini.

Stella ameyasema haya septemba 23 mwaka huu kwenye viwanja vya maonyesho EPZA bombambili mkoani Geita wakati akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uhimu wa watanzania kuwa na Bima kwenye maeneo mbalimbali.

” kumekuwa na muamko mdogo wa ukataji bima kwa wachimbaji ambapo natoa rai kwao kuchangamkia fursa hiyo kutokana na umuhimu wa bima hiyo.”Amesema Meneja

Ameongeza kuwa katika maonyesho hayo pia wanaeendelea kutoa elimu ya ukataji wa bima ya maisha, bima ya ajali ambayo itamsaidia mchimbaji pale ambapo anaweza kupata madhara katika shughuli zake za uchimbaji hivyo NIC kupitia bima yake ya ajali kwa ajili ya wachimbaji itaweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida.

Nakuongeza kuwa endapo itatokea bahati mbaya amefariki warithi wake wanaweza kufidiwa na kuendeleza shughuli zao zakiuchumi.

Amefafanua kuwa pamoja na kutoa elimu ya bima pia wanatoa elimu ya uwekezaji ambayo inamhakikishia mchimbaji au mtu mwingine yeyote kuwa ukipatwa na janga lolote lile familia ikiwemo watoto wataendelea kusoma .

“Katika maonyesho haya tumekuja kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto kama magari,pikipiki na bajaji tunatoa elimu hii ili hao wasafirishaji waweze kukata bima hizo na kuepusha ajali ambazo zinaweza kuwatokea ikapelekea magari yao kutokutengenezeka kabisa sababu yakutokuwa na bima wakikata bima na NIC Insurance tutawalipa ndani ya siku saba na taratibu zote tunafanya kulingana na miongozo ya kimataifa ndiyo maana tunalipa ndani ya siku saba”amesema Meneja Stella .

Pia ameongeza kuwa NIC wameweza kufanya mabadiliko makubwa kwa kipindi kifupi ambapo wanatembea kifua mbele kuwa wana uwezo wakulipa madai ndani ya siku saba.

Aidha ametoa wito kwa wakazi wa Geita katika kipindi hiki cha maenesho kutembelea banda hilo kupata elimu mbalimbali kuhusu bima