May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi NSSF afungukia huduma zao mbele ya Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko

Mkurugenzi wa Mfuko wa Nssf Masha Mshomba akimpa maelezo Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko mara baada ya kutembelea Banda na Nssf kwenye uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya madini yanayoendelea mkoani Geita

Na David Johntimesmajira online Geita

MFUKO wa Hifadhi wa Jamii NSSF umesema kuwa Katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuongeza thamani ya Mfuko huo kutoka Trilioni 4.8 Hadi kufikia shilingi Trilioni 7.6 kwa hesabu zinazoendelea kukaguliwa Hadi hivi sasa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Hifadhi hiyo Masha Mshomba mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko alipotembelea Banda hilo nakutoa pongezi Kwa NSSF kwa hatua kubwa waliyopiga.

Mshomba alimweleza Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa wamefanikiwa kuongeza thamani ya Mfuko Hadi kufikia kiasi Cha shilingi Trilioni 7.6 nakwamba hiyo ni hatua kubwa kufikiwa.

“Thamani ya Mfuko imeendelea kukua kwa kasi tukizungumzia mahesabu yaliyokaguliwa hadi mwaka jana Juni,tuliuwa na mahesabu ya shilingi trilioni 6.08,lakini kwa mwaka huu mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu hesabu ambazo bado zinaendeea kukaguliwa thamani ya Mfuko ni shiingi triioni 7.6″amesema na kuongeza kuwa
“Ni ukuaji mkubwa sana hasa ukizingatia kwamba kabla Rais Samia hajaingia madarakani thamani ya mfuko ilikuwa ni shiingi triioni 4.8 tu.”

Akizungumza kuhusu ushiriki wao kwenye maonesho hayo ya Madini amesema wapo kwa sababu ya kuelimisha wadau na wananchi kwa ujumla ilinwaweze kujiunga na Mfuko huo Ili kuendelea kuongeza wananchi na thamani ya Mfuko.

“Katika maonyesho haya tumekuwa na mafanikio makubwa ,tumeongeza wachangiaji wa NSSF ambapo kwa mkoa wa Geita tunakusanya shilingi bilioni 96 ,lakini wakati Rais Dkt Samia anaingia madarakani kwa mkoa huu tulikuwa tunapokea michango ya shilingi bilioni 26 tu,Amesema

Nakuongeza kuwa “Tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo.”amesisitiza

Pia amesema .Mfuko kwa ujumla tumekuwa pia na ‘perfomance’ nzuri sana ambapo mwaka unaoishia Juni 2023 thamani ya michango ilikuwa shilingi Trilioni 1.66 na shilingi Trilioni 1.48 kwa mwaka ulioishia Juni 2022 .