Na Esther Macha, Timesmajira Online, Chunya
MBUNGE wa Lupa, wilayani Chunya, mkoani Mbeya Masache Kasaka amesema kuwa kutokana na changamoto ya uhaba wa walimu wa shule ya msingi kibaoni yenye watoto wenye ulemavu analazimika kuishawishi Serikali kuajiri wataalam wa lugha za harama ili kuwezesha kundi hilo kupata elimu.
Kasaka amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni kutimiza mwaka mmoja tangu wananchi wampe ridhaa ya kuwatumikia na kuwawakilisha bungeni..
Amesem kuwa licha ya Serikali kutenga fedha zaidi ya Sh 900 milioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari wilayani humo bado kuna changamoto ya walimu wa lugha za harama
“Hii ni changamoto katika shule hii ya Kibaoni ni kubwa kutokana na ukubwa wa Wilaya yetu ,shule hii inahudumia watoto wenye ulemavu wa viungo,mtindio wa ubongo,watoto wenye ulemavu wa kusikia ,wilaya inafanya mikakati kupata walimu wa watoto wenye ulemavu wa kusikia”amesema Mbunge huyo.
Masache amesema kuwa hawana walimu kwa ajili ya viziwi na kwamba kwa upande wa shule ya msingi Lupa kuna shule moja ambayo sio maalum kwa ajili ya walemavu ila inatumika kwa eneo la Kipambawe kwani imeweza kusaidia kwani huko nyuma wazazi waliokuwa wakizaa watoto wenye ulemavu walikuwa wakiwaficha ndani uwepo wa shule umesaidia.
Aidha Mbunge huyo amesema kwamba uwepo wa shule hiyo umeweza kusaidia wazazi na walezi walio wengi wameanza kuwatoa ndani watoto wenye ulemavu ambao walikuwa wakificha wamepata mwamko wa kuwapeleka shule .
“Hapa shule wanapewa chakula bure walau inasaidia wazazi na walezi kuwa na mwamko ,bado kuna shida ya walimu wa kuwahudumia hawa watoto kwani wanaowahudumia ni walimu wa kawaida tu sasa tunatamani ingekuwa rasmi kwa walemavu tu wapatikane walimu ambao wapo kwa ajili ya walemavu hawa walimu wanajua jinsi gani ya kuwalea watoto wenye ulemavu inatakiwa kuwa mzazi kabisa,lakini kwa hawa walimu wa kwetu ambao wapo kwa ajili ya ajira mfano mtoto amejisaidia inakuwa ngumu kwake”amesema Masache.
Hata hivyo Masache amesema kwanza ilikuwa kuwatambua watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Chunya kwanza na kwamba changamoto kubwa ilikuwa kutotangazwa ajira hivyo wataongea na halmasahauri kupata walimu ambao watajitolea kwa kuwapa posho kidogo wanakuwa kama wanajitolea.
“Mkakati wa muda mrefu ni kuiambia serikali inapotoa ajira kwa walimu iangalie pia walimu kwa ajili ya kufundisha watoto wenye ulemavu hasa watoto wenye ulemavu wa kusikia ambapo kwa wilaya chunya hakuna walimu wa watoto wenye ulemavu wa kusikia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Saimon Mayeka amesema kuwa walilazimika kuanzisha shule hizo ambazo hazikuwa rasmi kwa ajili ya watoto wenye ulemau ili wazazi wapate msukumo wa kuwapeleka shule watoto wao,na kwamba kwa mwaka huu wanafikiria kutenga bajeti kutoka wizarani ili kusaidia shule hizo.
Aidha Mayeka alisema kutokana na uhitaji mkubwa kwa wilaya hiyo wameanza mikakati ya kuanzisha shule nyingine ya watoto wenye ulemavu katika Mji wa Makongolosi wilayani hapa .
“licha ya wizara pia kuweka bajeti kidogo ila upande wetu wa bajeti ya mkaa tumeongeza ushuru ili kuweza kuhudumia shule hizi fedha itatoka kwenye ushuru wa mkaa ,tuna kuni kubwa la watu wenye ulemau wa kusikia tunajipanga kuwapata ili waende shule kwa kutumia bajeti yetu kwa kutafuta walimu ambao watasaidia kufundisha watoto hawa kwa kuwalipa posho kidogo”amesema Mayeka.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi