May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah alilia mikopo ya Serikali wapatiwe Bodaboda wa Segerea

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,ametoa kilio chake kwa Serikali akimtaka Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, mikopo ya Serikali ikitoka wawezeshwe Vijana wa Bodaboda wa Jimbo la segerea.

“Kilio changu maafisa Usafirishaji Vijana wa Bodaboda waliopo Segerea wawezeshwe mikopo ya Serikali itakapotoka ya asilimia kumi ya Mapato ambayo ilikuwa ikitolewa ngazi ya Halmashauri “alisema Bonah.

Mbunge Bonnah alisema katika Jimbo hilo kuna vikundi vingi vya Bodaboda vilivyosajiliwa lakini hawajapatiwa mikopo ya Serikali iliyositishwa.

Aidha alisema katika jimbo hilo vikundi vingi viliandikishwa lakini hawakupata mikopo,na vipo vichache vilipata mikopo hiyo ya Serikali ambayo aina riba lakini hawakurejesha fedha za Serikali .

Alisema kwa kiasi kikubwa Bodaboda katika jimbo hilo wanaitaji fursa hiyo ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi kwani wengi waendesha pikipiki wanazo wanarejesha fedha kwa mikataba.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Omary Kumbilamoto alisema, halmashauru hiyo imetenga zaidi ya sh.bilioni 6.4 kwaajili ya mikopo ya asilimia 10 iliyokuwa akitolewa kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu na kwamba kama itaanza kutolewa basi vikundi hivyo vya bodaboda vitapewa kipaumbele.

“Nifedha ambazo zinasubiri
utaratibu . Rais atangaze tuendelee na utaratibu wa awali au utaratibu mwingine,” alisema Meya Kumbilamoto.

Alisema vikundi hivyo vya bodaboda Jimbo la Segerea ambavyo bado viko hai vitapewa kipaumbele pindi mikopo hiyo itakapoanza tena kutolewa kwa maelekezo ya serikali.