November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonah aiweka mtegoni Kamati ya ujenzi ya kituo Cha polisi

Na heri Shaaban, TimesMajira Online, Segerea

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli,ameiweka mtegoni Kamati ya Ujenzi wa Kituo Cha Polisi Segerea iliyokabidhiwa pesa Mabati na nondo kwa ajili ya kutekeza mradi wa kituo cha Polisi Segerea daraja C

Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli, alitoa kauli hiyo Leo katika ziara yake Jimbo la Segerea kukagua Miradi ya maendeleo pamoja na vituo vya Afya.

“Serikali ya awamu ya nne nilikuja katika Kata ya Segerea na Waziri Masauni ,Mkuu wa Majeshi wakati huo tukichagia pesa ,Mabati na nondo katika harambe ya ujenzi wa kituo cha Polisi lakini mpaka Sasa ujenzi wake umekwama ” alisema Bonah.

Mbunge Bonah alimwagiza Afisa Mtendaji wa kata Segerea kuunda Kamati kufatilia pesa za ujenzi na Mabati na nondo zimekwenda wapi mpaka Sasa ambazo zilikuwa zinajenga kituo hicho Cha kisasa daraja C “alisema Bonah

Jimbo la Segerea lina Kata 13 ndio Jimbo lenye Wakazi wengi Wilaya ya Ilala lakini hakuna kituo Kikuu Cha Polisi mikakati ya Mbunge wa Jimbo hilo imefanikiwa kupata eneo kwa ajili ya ukeketaji wa kituo cha Polisi ambapo ukeketaji wa ujenzi wake umekwama Kamati ya Ujenzi kudaiwa kushindwa kuendeleza ujenzi huo.

Katika ziara hiyo Mbunge Bonah alitembelea Kata ya Segerea kuangalia ujenzi wa kituo cha Afya Kata ya Kinyerezi kuangalia ujenzi wa kituo cha Afya na daraja la kwa Masisita Pamoja na Ujenzi wa Kituo Cha AFYA Kiwalani .

Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli alisema ziara hiyo ni sehemu ya ziara yake Jimbo la Segerea kufatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kufatilia miradi ya Chama .