May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbatia:Kujiuzulu kwa Ndugai ni batili

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

IKIWA ni Siku moja imepita tangu Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ajiuzulu, Chama Cha NCCR _Mageuzi kimejitokeza hadhari na kudai kujiuzulu kwake ni batili na kumekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 149(1)(C).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, James Mbatia wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mbatia amesema nafasi ya Spika wa Bunge na mhimili wa Bunge ni zao la katiba ya nchi.

Amesema utaratibu uliopo wa namna ya Spika kujiuzulu upo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 149(1)(C) na kueleza kuwa iwapo mtu huyu ni Spika au Naibu Spika wa Bunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha katika Bunge.

Mbatia amesema mazingira ya kujihuzulu kwa Spika Ndugai ni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni matamshi kuhusu deni la Taifa na kueleza kuwa sio sababu tosha ya kumfanya aachie nafasi yake ya Uongozi.

“Tukio la Kujiuzulu kwa Spika Ndugai lina uzito kwani ni kiongozi wa mhimili wa dola yaani Bunge anajiuzulu kwa kuandika barua kwa katibu Mkuu wa Chama chake cha Siasa tangu lini Chama cha Siasa kiakwa na Mamlaka ya juu yanayozidi katiba ya nchi?alihoji Mbatia

Na kuongeza kuwa
” Tukio la Kujiuzulu kwa Spika Ndugai ni kichocheo cha kukamilika mchakato wa kupata katiba mpya “amesema Mbatia

Alifanunua kuwa nafasi ya Spika haipo kwa matakwa ya Chama cha Siasa na kueleza kuwa kama Chama hicho kilitaka kumuondolea uspika kingemvua uanachama ili tiketi iliyompa fursa ya kugombea uspika iondoke.

Mbatia amesema endapo uvunjifu wa katiba utaendelea NCCR_Mageuzi itaendelea kuzungumzia suala hilo na kueleza kuwa hatua kali zitachukuliwa ikiwa na pamoja na kwenda kuiomba mahakama kutumia ibara ya 108 .

“Tutaweza kwenda mahakamani kwenda kuzuia mchakato wowote utakaoendelea wa kuvunja katiba kwa upande wa mchakato huu uliofanyika ni batili”

Na kuwa kwa sasa wanashauriana na wanasheria wa Chama hicho na kueleza kuwa wakikubaliana na hali hiyo tutaiomba mahakama iweze kuingilia kati”alisisitiza Mbatia

Alibainisha kuwa NCCR _Mageuzi ni chama ambacho kimekuwa kikijikita katika hoja na kueleza kuwa katika bunge la mwaka 1995/2000 ilifanya kazi chini ya mfumo wa Vyama vyingi vya Siasa .

Aidha aliwaomba Wazee, na Viongozi wastaafu, Viongozi wa dini kwa pamoja wasimame na kukaa kwa pamoja ili kuweza kulishauri Taifa na kukaa pamoja kwa maslahi.

Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR_Mageuzi Taifa James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kuhusu suala nzima la kujiuzulu kwa Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai