April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mawakala wa Bima zaidi ya 500 kupata mafunzo

Jackline Martin, TimesMajira Online

BENKI ya NBC kwa kushirikiana na kampuni ya BIMA Jubile Allianz imesema wataendelea kutoa elimu ya BIMA kwa mawakala nchini, ambapo hadi kufikia mwezi wa sita wanatarajia kutoa mafunzo kwa mawakala wasiopungua 6000 lengo kuu ikiwa ni kuongeza urahisi wa upatikanaji wa Bima nchi Nzima na pia kulikuza soko la Bima

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Bima Kutoka NBC, Benjamin Nkaka wakati wakikabidhi vyeti kwa mawakala wa Benki ya Biashara NBC zaidi ya 100 waliofanya mtihani na kufaulu ikiwa ni wiki chache zilizopita baada ya kupatiwa mafunzo ya uuzaji Bima Kukamilika.

Nkaka alisema matarajio yao kwa wahitimu ni kutoa huduma bora kwa wateja, kuwapa elimu na kuhakikisha kuwa wanasogeza Zaidi huduma ya BIMA kwa wateja wao.

“Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz kushirikiana na Benki ya NBC, ilichagua mawakala wa huduma za kifedha, kuwadhamini na Kuwapeleka mafunzo ya muda mfupi katika chuo cha Africa College of Insurance and Social Protection kwaajili ya kupatiwa elimu ya Bima.”

Alisema NBC na Jubilee Allianz wataendelea kuwa Bega kwa Bega kuwapa msaada wa kitaalamu wahitimu hao muda wote kwani zoezi hilo litakuwa ni endelevu.

Àq1111q1

Naye Meneja Mkuu msaidizi wa Jubilee Allianz, Abullatif Suleiman, alisema hadi sasa ukuaji wa bima katika soko ni mdogo ndiyo maana Jubilee Allianz pamoja na Benki ya Biashara NBC wakawaingiza mawakala katika huduma hiyo ya kuuza Bima.

“Sisi kama Jubilee Allianz tunaona ni fursa kubwa, nyinyi mnapokea wageni wengi katika vituo vyenu na katika hili hatutowaacha pekeenu, sisi na NBC tutakuwa tunawapitia katika vituo vyenu kuhakikisha mnaweza kuuza na kutatua changamoto mnazokutana nazo.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo na taaluma kutoka ACISP, Ansium Anseum alisema wataendelea kuwafundisha na kuwawezesha mawakala hao ili waweze kwenda kutoa huduma bora za bima nchini kote. Aidha aliwataka wahitimu hao kwenda kutoa huduma iliyo bora kwa kuzingatia maadili ya kazi na misingi iliyowekwa kwani huduma ya bima inahitaji uwazi na ukweli kwa mteja.

Meneja wa mawakala wa Bima kutoka NBC, Janeth Sindano alisema kwa sasa wao kama NBC wana zaidi ya mawakala 9500 ambao wapo nchi nzimawakiwemo mawakala wakuu, wa kawaida na mawakala wa kati ambao watakua nao bega kwa bega kwenye zoezi zima la uuzaji wa bima kupitia jubilee allianz.