May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Wilaya ya Kahama , Anamringi Macha akiongea na wandishi wa habari wilayani hapa kuhusu maswala ya usalama .Picha Patrick Mabula.

Mauaji ya watu 4 na watu wasiojulikana yachunguzwa

Na  Patrick Mabula, Kahama.

SERIKALI wilayani Kahama imesema inafanya uchunguzi  juu ya tukio la miili ya watu wanne waliouawa  kisha kutupwa katika mto uliopo kijiji cha Mwabomba kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu  na kukutwa ikiwa imeharibika vibaya ili sheria ichukue mkondo wake.

Mkuu wa wilaya ya Kahama , Anamringi Macha alisema miili ya watu hao waliouawa na watu wasiojulikana ilibainika jumapili iliyopita katika mto huo uliopo karibu na machimbo ya dhahabu ya Mwabomba  ikiwa imeharibika vibaya  huku sura zao kutotambulika .

Macha alisema serikali  kwa kutumia vyombo vyake vya dola inafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu waliofanya  kitendo cha  mauaji hayo na kuitupa miili hiyo katika mto huo unaotenganisha wilaya ya Kahama na wilaya ya Mbogwe mkoa wa Geita waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.