January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matukio yaliyosisimua Novemba 27, 2020

Mwalmu akiwa amevalia barakoa huku akikagua daftari la mmoja wa wanafunzi katika Shule ya Sangharsh Vidya Kendra iliyopo katika kitongoji cha makazi duni mjini Jammu, India juzi (Picha na AP).

Wakazi wakiendelea na pilikapilika huku wengine wakioga na kuchota maji katika Kijiji cha Rodriguez jimboni Rizan, Ufilipino. Kijiji hicho kiliharibiwa vibaya na kimbunga Vamco juzi. (Picha na Reuters).
Wafanyakazi wa manispaa wakishirikiana kuweka mti wa Krismasi eneo la Red Square ambalo lina makumbusho ya kihistoria kushoto na ofisi za Jimbo la Gum kulia. Tukio hilo lilifanyika jana mjini Moscow nchini Urusi ikiwa ni maandalizi ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya. (Picha na AP).
Mwanamke raia wa Palestina akiwa amesimama na watoto wake mbele ya nyumba yao iliyopo katika makazi duni Kusini mwa Ukanda wa Gaza juzi. (Picha na AP).
Maafisa wa Jeshi la Polisi wakiwa wamejipumzisha huku wakitumia simu zao karibu na eneo la jumba la mfalme mjini Bangkok, Thailand wakati wakiendelea na operesheni ya kudhibiti maandamano ya raia dhidi ya Mfalme Maha Vajiralongkorn wakishinikiza mali za ufalme huo zirudishwe chini ya utawala wa raia. (Picha na Reuters).
Maafisa wa Jeshi la Polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi wahamiaji kutoka Morocco baada ya kuwasili katika Pwani ya Kisiwa cha Canary nchini Uhispania juzi. (Picha na AP).