Barafu ikiwa imezingira magari katika eneo la maegesho lililopo mjini Bakhchisaray, Crimea juzi. (Picha na REUTERS). Watu wakitembea karibu na makumbusho mjini Washington DC, Marekani juzi huku bendera zikipepea nusu mlingoti ikiwa ni ishara ya kuomboleza vifo vya Wamarekani 500,000 waliofariki kwa virusdi vya Corona. (Picha na REUTERS). Wanandoa waliojitambulisha kwa jina la Bibi na Bwana Lim wakipatiwa chanjo dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19) katika Ukumbi wa Senja-Cashew Community nchini Singapore juzi. Nchi hiyo imetangaza kuwa watu wote wenye umri wa miaka 70 na kuendelea watakuwa wamepatiwa chanjo hiyo ndani ya mwezi Machi, mwaka huu. (Picha na THE STRAITS TIMES/GAVIN FOO). Kondoo wakiwa wanakatiza katika mitaa ya Llandudno, Wales nchini Uingereza juzi. (Picha na REUTERS). Kikosi cha uokoaji kikitafuta wachimbaji waliofukiwa katika machimbo waliyokuwa wanachimba kinyume cha sheria yaliyopo Kijiji cha Buranga, Parigi Moutong Regency, Sulawesi jana. Ajali hiyo ilisababishwa na mwamba kuporomoka. (Picha na AFP). Post Views: 1,297 Continue Reading Previous Matukio yaliyosisimuaNext Rais Mwinyi aelekea Msumbiji More Stories CHAGUO LA MHARIRI (PICHA) Kapinga akagua banda la Wizara ya Nishati August 24, 2024 Judith Ferdnand CHAGUO LA MHARIRI (PICHA) Mwenyekiti ACT-Wazalendo akutana na viongozi wa chama hicho taifa March 8, 2024 Judith Ferdnand CHAGUO LA MHARIRI (PICHA) Othman ashiriki kikao kamati kuu ACT-Wazalendo March 3, 2024 Judith Ferdnand
More Stories
Kapinga akagua banda la Wizara ya Nishati
Mwenyekiti ACT-Wazalendo akutana na viongozi wa chama hicho taifa
Othman ashiriki kikao kamati kuu ACT-Wazalendo